Msaada: Mgogoro wa aridhi mapiga bagamoyo

kidodosi

JF-Expert Member
May 1, 2013
2,290
1,379
Mimi na jamaa zangu wawili, tumenunua Aridhi MAPINGA kijiji cha UDINDIVU wastani wa hekali moja kila mmoja kutoka Serikali ya kijiji,kila mmoja alilipa shilingi milioni tano{5,000,000} mwaka 2010.
Mwaka 2013 mwenyekiti wa kijiji alitupa taarifa kwamba kuna mtu kajitokeza anadai yeye ni mmiliki wa hilo eneo kwahiyo shauri walilipeleka baraza la kata, Baraza likatoa maamuzi kwamba serikali ya kijiji ndiyo wamiliki wa eneo;

Kutokana na maelezo ya mwenyekiti wa kijiji jamaa anayedai kwamba ni mmiliki alikata rufaa mahakani Kibaha na 2015 ameshinda kesi na amemilikishwa eneo.
Kwahiyo basi mwenyekiti wa kijiji anasema kwa kuepusha usumbufu anatupatia eneo lingine.

WASI WASI:
1.Mpaka sasa hajanionesha nyaraka yoyote ya maamuzi ya baraza la kata wala Mahakama ya Kibaha.

2.Sijawahi kukutanishwa na mtu anayedaiwa kuwa mmiliki wa hilo eneo.

3.Eneo tulilouziwa kwa sasa limekatwa katwa viwanja na kupewa watu wengine, mwenyekiti wa kijiji anasema mmiliki amewagawia ndugu zae.


Naomba ushauri :
Nifanyeje ili kuhakikishiwa kwamba hilo eneo tunalopewa kama fidia halina mgogoro?

 
Back
Top Bottom