salute comrades[emoji868]
Husika na kichwa cha habari hapo juu, nina dada yangu kipenzi anayetarajia kumaliza kidato cha nne mwaka huu. Ila ktk hali isiyo ya kawaida mwili wake ilianza kupata mabadiliko na kuonekana mchovu wa mwili, jambo lililopelekea hata mahudhurio yake shuleni siku za hivi karibuni kuwa ya kususua,kiukweli tulianza kumtilia mashaka, na leo tukampeleka maabara na kama tulivyotarajia kweli kweli ni mjamzito,
Sasa swali ni je hivi hii hali ya ujauzito itamfanya akose masomo yake mazima. au anaweza kubakia nyumbani akijisomea na siku ya NECTA akaenda kufanya paper au ile hali ya tumbo kuwa kubwa haitomwezesha kufanya mtihani na ikizingatiwa ktk kipindi hiki cha mitihani mimba itakuwa na miezi8, na ikitokea akatakiwa azae kwanza je, kuna nafasi ya pili ya yeye kupata haki yake ya kusoma baada ya kujifungua…
Nitafurahi kama matachangia kama ilivyo mada na sio kukejeri maana hii ni issue serious kabisa, karibuni…