Msaada;mchumba wangu anaumwa nini?

Msaada;mchumba wangu anaumwa nini?

Sukari Yenu

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2014
Posts
1,698
Reaction score
1,260
Habari wana jamvi, mimi ni kijana na nina mchumba wangu wa muda mrefu kidogo ingawa tuna misukosuko mingi sana. Ili ujue tatzo la mchumba wangu huyu, naomba usome mlolongo wa matukio ktk uhusiano wetu kwanza.

Tulifahamiana mwanzoni mwa mwaka 2011 tukapendana. Mwaka huo huo mwezi Octoba nilienda kuanza chuo kikuu mjini Dodoma hivyo nikamwacha mtaani.

Yeye alikua anaishi na dada yake jirani na nyumbani. Hakufurahia kuondoka kwangu, na alijua nitamwacha na kufuata mabinti wasomi yeye ana elimu ya msingi tu.

Aliniambia nimuachie ujauzito na nimtambulishe nyumbani, wazo ambalo mimi sikuliafiki. Nikaondoka akiwa amekasirika sana mpaka akawa hapokei simu zangu lakin alikuja kunielewa tukaendelea.

Kuna kipindi alienda kwao wakataka kumuozesha akakataa kwa sababu yangu na nilimtumia pesa ya nauli akatoroka.
Alipotoroka alipitia Moshi kwa ndugu zake wengine ambako alipata matatizo ya kubakwa na mtu aliyekua akimsumbua sana kumtaka kimapenzi, baada ya kumlaghai.

Tukio lile lilisababisha,mimba ambayo ni mtoto aliyenae kwa sasa. Haukuchukua muda alirudi jijini Dar tulikutana na tukawa tunashare kitanda lakin hakuniambia kama alibakwa. Badae akabaini ujauzito na alijua fika ni wa yule jamaa wa Moshi ila akaniambia ni wangu.

Nilikua mgumu kuukubali na tuligombana sana cause nilikua nafuatilia tarehe zake. Wakati huo hakua na msaada wowote hapa jijin cause dada yake alisharudi kijijini kwao ila bado alikua anaweza kwenda kazini kwake (waiter katika mgahawa ) nami pia nikimsaidia matumiz madogo madogo na nikilea mimba fifty fifty.

Mara nyingi alitishia kujiua endapo ningemwacha. Aliniomba fedha nyingi ya nauli na matumiz arudi kwao akajifungu, mimi nilimshauri abaki Dar cause mama yangu yupo atamhudumia lakini alikataa, akazidi kunipa mashaka.

Pesa nilimpatia. Baada ya kumbana sana mimba ilipokua kubwa na akagundua nimejua sio yangu akaacha kuwasiliana na mimi kabisa wakati huo nilikua masomoni Dodoma.

Kumbe nilipompa pesa hakuondoka kwao akahama alipokua anakaa na kwenda sehemu nyingine, ndipo nikagundua nimeingizwa mjini ila kwa sababu nilikua nahudumia mimba fifty fifty sikuumia sana.
Alipoenda kujifungua alipata matatzo zaidi, alilazwa amana baadae akapoteza faham akawa referred muhimbili.

Dadake alinipigia simu kunipa taarifa za mtoto wa kike aliejifungua na kwamba anahitaji pesa za matibabu ikiwepo chupa 1 ya damu. Hapo alishaongezewa 1 ikawa inahitajika nyingine. Mimi nikamjibu sitoi hiyo pesa na arudi kumuuliza mdogo wake baba wa mwanawe.

Yule dada alishtuka cause hata yeye alimficha siri ile na alidhani mimi ndie baba wa mtoto. Aliporudi wodini na kumbana mdogo vizuri binti akasema ni kweli mimi sio muhusika wa mimba ile na hakua tayar kuelezea tukio la kubakwa

. Dada alipata hasira akamuacha mdogo wake muhimbil bila msaada wowote kwa wiki 1 na alipoenda alikuta bado yuko vile vile bila msaada na damu yazidi kushuka ila alimchukua mtoto na kurudi nae home.

Siku moja mgonjwa alikamatwa akitaka kutoroka, alilia sana na akang'ang'aniza aruhusiwe aondoke. Madaktar wakampa vitabu akasaini wakamwacha. Akamchukua mtoto na kumpeleka Moshi kwa familia ya mzazi mwenzie.

Walimpa pole na kumlaumu kijana wao tu, wakamwomba bint abadili dini aolewe na mbakaji wake nae akakataa kubadili dini. Au amuache mtoto na wamlipe pesa atakayo akakataa pia. Alichotaka ni matunzo ya mtoto tu. Baada ya kuona familia ya mbakaji haieleweki akajiondoa zake na kwenda Babati kwa ndugu zake wengine na mwanae.

Akajipanga akarudi mjini, maisha yakamuia magumu alifumwa akimbana pumzi mtoto ili afe asiendelee kuteseka. Ni mkatili sana huyu binti. Kipindi hicho chote tangu akate mawasiliano na mimi tulikua hatujawahi kuonana. Mwakajana mwishoni tumeonana na akaniomba msamaha.

Sikumsamehe kwanza, nilitaka kujua kwann alinisingizia mimba. Ndipo alinieleza chanzo cha mimba ile na masahibu yote yaliyomkuta mpaka hapo alipo na kuongeza kuwa alifanya vile ili nisimwache coz alikua bado ananipenda sana. Akaongeza tena kuwa hata jina la pili la mwanawe ni langu mimi na hatolibadilisha.

Nilimwonea huruma sana na maisha anayoishi sasa ni magumu sana sana, plus incidence ya Muhimbili n.k nikajionea sina haja ya kisasi nae. Nimemsamehe. Ila nikamuomba afike nyumbani amuombe radhi mama yangu pia cause anajua kila kitu.
To cut the story ni kwamba ameniomba turudiane na kudai ananipenda sana.

Nikamtega, nikamkubalia kizushi ili nione kama kweli kabadilika na sijala tunda lake mpaka leo hii tangu Novemba mwaka jana aliponiomba turudiane. Kiufupi hatujalala tena pamoja tupo kaka na dada tu.

Sasa kinachonishangaza ni kwamba amekua mtu wa kulalamika sana maisha magumu, anaweza kuniahidi atakuja nyumbani kwangu nilikopanga haji, nikimuuliza anadai kazi nyingi sana. Anadai mtoto anasumbua anaumwa umwa sana cause ana pumu.

Anadai Huko nyuma alidhani mi nimemfanyia ushirikina apate tabu ndio maana akanitafuta aombe radhi. Somtym anahusisha matatizo yake na wazee wake kijijini aliowakimbia kuolewa. Kumbuka tangu 2012 hajarudi kwao baada ya kutoroka. Anawaza kurudi Irangi Kondoa kijijini kwao akaombe radhi wazee wake. Waliotaka kumuozesha ni upande wa mama yake.

Baba yake mzazi hamjui na mama yake amekufa siku nyingi. Kuna siku nimemkuta analia kwake kule na anadai laiti mama yake angelikua hai asingepata tabu zote hizo. Baba wa mtoto hawaelewani tena. Alitaka ahamie kwangu nimemkatalia.

Amekua mtu wa kukata tamaa ya maisha sana. Anaweza hata kuua yule mtoto au kujiua mwenyew yule. Yaani haeleweki tu. Je, nimrudie kiukweli kweli, mi napenda awe tu rafiki yangu tu cause ana attitude ya utafutaji pesa and I like that. Na mtu huyu anahitaji msaada gani?
 
Stori ndefu mpk nimechemka kuisoma.

Mwanzoni nilijua wewe ni she.. Hilo jina unalotumia kwa mwanaume.... hakyamama ni shida.

Ngoja watakuja vijana wenzako wakusaidie.
 
Stori ndefu mpk nimechemka kuisoma.

Mwanzoni nilijua wewe ni she.. Hilo jina unalotumia kwa mwanaume.... hakyamama ni shida.

Ngoja watakuja vijana wenzako wakusaidie.

Nakuomba soma tu ni story yenye majibu ya swali langu and it is very interesting, plz take time
 
Nakuomba soma tu ni story yenye majibu ya swali langu and it is very interesting, plz take time

Haya nimeisoma....

Niambie kwanza.... moyo wako unakutuma nini.... umrudie au umpige chini?

Tuanzie hapo kwanza.
 
Haya nimeisoma....

Niambie kwanza.... moyo wako unakutuma nini.... umrudie au umpige chini?

Tuanzie hapo kwanza.

Sitaki kumrudia. Jamii nayo haitaniangalia vema pia kwa sasa sipo tayar kuoa na yeye anataka ndoa. Nimemaliza chuo mwaka jana July, Mungu ni mwema nimepata kazi mwez September nahtaj kuwa single for somtym
 
Hapo kwamba alibakwa ndio amekudanganya. Hajabakwa huyo alitoa game kwa hiari.

Jambo lingine huyo mwanamke sio mkweli,hiyo kwangu ni point muhimu ya kumdiskolifai na kila kitu. Kama alitaka akusingizie mimba wakati anajua sio yako kwa maksudi bado unamuamini?

Hiyo ya kulia lia ni defence mechanism ya kutafta sympathy kwako ili umkubalie shida yake vinginevyo hana jipya,ni tapeli sema keshagundua wewe ni zombi akikwambia lolote unakubali.

Ok,nakushauri mdogo wangu achana na huyo binti,sio mtu mzuri kabisa.

Lingine mdogo wangu jitahidi uwe unaandika kwa aya,haiwezekani useme una elimu ya chuo kikuu uandishi wako uwe hivi.
 
Hapo kwamba alibakwa ndio amekudanganya. Hajabakwa huyo alitoa game kwa hiari.

Jambo lingine huyo mwanamke sio mkweli,hiyo kwangu ni point muhimu ya kumdikolifai na kila kitu. Kama alitaka akusingizie mimba wakati anajua sio yako kwa maksudi bado unamuamini?

Hiyo ya kulia lia ni defence mechanism ya kutafta sympathy kwako ili umkubalie shida yake vinginevyo hana jipya,ni tapeli sema keshagundua wewe ni zombi akikwambia lolote unakubali.

Ok,nakushauri mdogo wangu achana na huyo binti,sio mtu mzuri kabisa.

Duh!! Nimekua zombi tena? I took it easy kwanin tuwekeane visasi mimi nimemsamehe bure. Hili suala la kubakwa ndio sina uhakika nalo.
 
Sitaki kumrudia. Jamii nayo haitaniangalia vema pia kwa sasa sipo tayar kuoa na yeye anataka ndoa. Nimemaliza chuo mwaka jana July, Mungu ni mwema nimepata kazi mwez September nahtaj kuwa single for somtym

Orayt.... sasa ulikuwa unataka tukushauri nini? Huyu unasema ni mchumba wako, maana yake ushamtolea mahari, right?... Utaenda kudai mahari yako au??

BTW nimekusoma uko interested na yule binti wa miaka 30 anayetakiwa na baba yake aolewe ifikapo March..... vinginevyo baba yake atamgegeda mwenyewe..... Nakushauri kaza buti umpiku baba yake.

Huyu aliyebakwa naona huna tym naye tena maskini.. japokuwa umesema unampenda kwa kuwa ye ni mchacharikaji wa kutafuta njuruku.
 
Kumbe majibu yote unayo, fuata moyo wako
 
Mnh mkuu msaidie huyo dada km binadamu tu....cha kufanya labda umpe kamtaji afungue biashara yake mwenyewe ajitegemee au msaidie hata aingie shule hizi za ufundi then awe na maisha yake binafsi.......usijaribu kumuoa huyo kichwa chake kishakuwa messed up na hili life kiasi kwamba i dont think she thinks straight.........mmmmmmmmnh msaidie km binadamu km nilivyosema na pia uwe unaongea nae mara kwa mara ili awe na mtazamo chanya juu ya life....

Hio ya kubakwa ni Mungu ndie anaejua,mie siwezi kusema ni uongo kwa sababu watu wengi wanaobakwa huwa hawasemi mtu yuko tayari kusema alifanya mapenzi na mtu mimba ikaingia kuliko kusema alibakwa-huwa km wanajipunish kwa kufeel guilty/ni makosa yao wamebakwa......

Mwisho mkuu acha kutulisha chai,sasa km huyo dada alikuwa hospital na alikuwa na upungufu wa damu imekuwaje alivyojiondoa hospital bado akaendelea kuwa mzima???au alijiwekea mwenyewe damu mmnh...haya bwana
 
Dah!hii stori inachanganya kwa jinsi ilivyopangiliwa na lugha ilivyotumika,ila sio mbaya mana hatupo kwenye jukwaa la lugha.Uyo binti ukiendelea nae anaweza akakuletea matatizo ambayo mimi na wewe hatuyajui kwa sasa mana anaonekana ni mtu muongo na katili sana.
 
Ungekuwa mdogo wangu ningekuwasha kibao kimoja na kukuambia niondolee stori zako za kiduwanzi hapa. Unamhurumia umemzaa wewe? Eti ana attitude ya kutafuta pesa. Khaa
 
Orayt.... sasa ulikuwa unataka tukushauri nini? Huyu unasema ni mchumba wako, maana yake ushamtolea mahari, right?... Utaenda kudai mahari yako au??

BTW nimekusoma uko interested na yule binti wa miaka 30 anayetakiwa na baba yake aolewe ifikapo March..... vinginevyo baba yake atamgegeda mwenyewe..... Nakushauri kaza buti umpiku baba yake.

Huyu aliyebakwa naona huna tym naye tena maskini.. japokuwa umesema unampenda kwa kuwa ye ni mchacharikaji wa kutafuta njuruku.

Nimeandika mchumba ku-conquer attention za watu tu hapo. Hata kwao hawanijui mimi
 
Kaka kama kweli umemaliza chuo kikuu why unaandika hivi? si uwe unapangilia vizuri basi. Msaidie huyo dada kama alivyosema Jestina.
 
Last edited by a moderator:
KAma StoRi La ShIgonGo ViLe. SuKari yeNu# umetishaaa mcheki shigongo hapa mfAnYe KaZi pamoJa 0654187234
 
Orayt.... sasa ulikuwa unataka tukushauri nini? Huyu unasema ni mchumba wako, maana yake ushamtolea mahari, right?... Utaenda kudai mahari yako au??

BTW nimekusoma uko interested na yule binti wa miaka 30 anayetakiwa na baba yake aolewe ifikapo March..... vinginevyo baba yake atamgegeda mwenyewe..... Nakushauri kaza buti umpiku baba yake.

Huyu aliyebakwa naona huna tym naye tena maskini.. japokuwa umesema unampenda kwa kuwa ye ni mchacharikaji wa kutafuta njuruku.

story ya kutunga, ndefu, haina paragraph, haina mantiki

imejaa fiksi juu ya fiksi
 
Mchumba wako haumwi chochote...ila ni muzigo musito tu. Piga chini.
Sexy shape, baby face, sweat tongue=ATTITUDE YA BIASHARA, anauza vyote hadi yey mwenyw. Mara nying watu hawa ni Bar-maid, bussiness lady, hotelia, dancer n.k. HAWAOLEWI HAWA. ANAYEOA HAWA KAJISAHAU...kwambaa, ni cha wote. Xo, usiwe na wivu...na usipokuwa na wivu...ww ni chakaramu.

ILA ANAPOKUGEUZA WEW KUWA NDIO MTEJA WAKE BINAFSI...Badala ya kukuweka kweny nafasi yako ya bf, huyo ni musiba. HUWA CKU ZOTE DIRA YAO NI KUPATA KUTOKA kwa wanaume, na kuwekeza kwao. Yaan, mioyoni mwao wamesaini kwamba one day ataachwa coz anawahurumia wengi men! XO, SHE DIZAINI HIYO NI NYOKA FULANI HIVI...! Ni mpaka cku ifike akung'ate ndo utaelewa xomo. Vinginevyo twend tu mwendo wa mizinga, outing, shopping, na shida mbal mbal. Ukifeli kumpa anachotaka atakwambia una msaada gani??? Wakat msaada wake kwako ni "*K*"tu! UKISTUKA...PIGA CHINI FASTA. Na hawanaga machozi hawa. Akilia ni comedy tuuu ili akumalize.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom