ESCORT 1
JF-Expert Member
- Dec 7, 2015
- 1,368
- 2,890
Baada ya kukumbwa na upepo wa kutumbuliwa kibarua changu, hali yangu kiuchumi imeyumba mno kwani kwasasa mambo yangu mengi hayaendi, wale waliokuwa wananitegemea ikiwemo mama mkwe wangu siwatumii tena vijisenti. Sasa toka wiki iliyopita mama mkwe yupo hapa nyumbani akicheki menyu yenyewe inalegalega dagaa mchana kwa usiku.
Amenipa ultimatum, nimuache mwanae kwani ninamtesa mwanae na yeye kiujumla, amenambia kufikia mwisho wa mwezi huu niwe nimetoa talaka la sivyo ataenda kwa mganga kuniloga nife ili mwanae aolewe na wenye pesa. Wadau nifanyeje maana mama mkwe ndio huyo katoa kauli yake na kesho yeye anaondoka kurudi kijijini Buhigwe mkoani Kigoma.