mtu anapoomba ushauri wa ku activate windows unatakiwa umfundishe njia za kihalali za ku activate windows. unaponunua laptop unalipia hardware (laptop yenyewe) na software ambayo ni windows. windows ya bei rahisi ni around 80,000 na inaweza kuzidi hadi 300,000 inategemea na version.
unapomshauri mtu atumie kmspico ambayo ni njia ya wizi wakati ana genuine key chini ya laptop yake inamaana ni sawa na kumdhulumu huyo mtu 80,000 hadi 300,000 yake hivyo kitu cha kwanza unatakiwa umkague kama ana genuine key.
na si laptop zote zina key chini kuna laptop zinakuja na DOS na nyengine zinakuja na distro za linux kama ubuntu