Kwanza hongera kwa kuyapata maji.
Sina utalaam sana na open well, je umechimba umbali gani mpaka ukayapata maji? Hakikisha tu isije ikawa ni juu juu maana yawezekana ikawa maji machafu unayopata. Peleka sample ya hayo maji ikapimwe maabara kama haina wadudu wa kusababisha magonjwa. Vilevile maji yapimwe ili kujua viwango vya madini mbalimbali kwenye maji hayo ili kujua kama yanafaa kwa matumizi ya binadamu e.g kunywa au kupikia.
Kuhusu kuyafanya yawe meupe, tumia pampu iwe inayatoa nje mpaka yatakuwa meupe tu. Rangi ya maziwa inatokana na wakati wa uchimbaji.
Inaweza kukuchukua siku mbili tatu mpaka maji yawe meupe, unatakiwa uyapampu nje mfululizo mpaka yatakate.
Kama hali ya uchumi inakuruhusu itakuwa vizuri kama ukichimba "Bore Hole' kisima chako kitakuwa na usalama zaidi wa kiafya kuliko open well.