Habari wakuu, naomba msaada wa ushauri nataka nunua laptop kwa matumizi ya kawaida, ipi ni nzuri na naweza pata wapi kwa DSM ambazo c fake. Please, help me.
fake ni ipi kwanza kwa vigezo vyako? Maana usije ukawa na kasumba kuwa ya kutoka china ni fake. Hapo unaweza kuuziwa laptop yenye label made in USA kumbe imetengezewa China na bado ukagongwa bei. Hata laptop za UK USA nazo zaweza kuwa fake tena mbaya zina mpaka fake price. teh teh teh
Habari wakuu, naomba msaada wa ushauri nataka nunua laptop kwa matumizi ya kawaida, ipi ni nzuri na naweza pata wapi kwa DSM ambazo c fake. Please, help me.
Used or Brand?? na unapendelea ya kampuni gani? Dell. Hp, Toshiba Acer, Eee, Fijitsu Siemens .... which one, ni pesa yako unatoa na wewe ndo utakuwaq unatumia tupe maoni yako
Used or Brand?? na unapendelea ya kampuni gani? Dell. Hp, Toshiba Acer, Eee, Fijitsu Siemens .... which one, ni pesa yako unatoa na wewe ndo utakuwaq unatumia tupe maoni yako
Mkuu, me nakutegemea wewe zaidi, cjawahi kuwa na laptop so naomba unishauri brand ipi ni nzuri na naweza pata wapi kwa dsm whether ni mpya au hata used, asante.
budget yako ni shilingi ngapi kwani
mpya au hata used, asante.
Used or brand ndo nini.? Laptop zote hata used zina brand.
Nunua Toshiba. au HP. Toshiba ni imara zaidi. HP hata ikiharibika rahisi kupata spare kuliko brand nyingine zote.
Sasa kulingana na matuzi na uwezo wako nenda katafute model inayokufaa kwa bran hizo
HP wanyo makundi matatu Pavalioni Mini na envy HP Home Laptop PCs at a glance - HP Home & Home Office products
Toshiba wana makundi kamamatano Toshiba Direct | Laptops, Notebooks, Accessories, Electronics & Projectors home , gamer ,wide screen proffesional thin and light
So nakushauri nenda na satelite model ya Toshiba. though sijajua matumizi yako na bajeti yako
nunua yoyote hile lakini usinunue zile wanaita netbook laptops computing power yake siyo faster inababaisha. ukitaka kuenjoy zaidi nunua ambayo ni core 2 core duel powers au zaidi hizo ndo nikama mpya mpya na sikuhizi zina bei poa. kama unanunua used more than 12 months usiguse kabisaaaa vilaptop vingi vina useful life of miezi 18 utakuwa na umebakiwa na kama miezi 6 ya hiyo laptop kukusumbua halafu mother bord ife kabisaa hiyo ni common problemo. ushauri zaidi nunua mpya kama unauwezo zilizotumika mara nyingi hazikai sana na kufanya kwake kazi ni kulegalega tuu kwa sababu ya milage
Habari wakuu, naomba msaada wa ushauri nataka nunua laptop kwa matumizi ya kawaida, ipi ni nzuri na naweza pata wapi kwa DSM ambazo c fake. Please, help me.
Ndugu, ukitaka laptop mpya kabisa kwa Dar zinapatikana, na ni bei rahisi ukilinganisha na nje ya nchi, cha muhimu ujue matumizi yako ya hiyo laptop, iwapo ni kwa kazi za kawaida za kuchapa na kusoma ujumbe au kazi nyingine ambazo zinahitaji software na hardware tofauti tofauti ili kufanikisha kazi zako. Mfano, kama kazi ya laptop yako ni kuchora michoro mbalimbali kwa kutumia AutoCAD ama software nyingine, au kama ni music production au video production, bila shaka utahitaji yenye spidi kubwa na uwezo mkubwa wa kutunza kumbukumbu na kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja.
Mie nina HP pavilion DV6000 Series, niliinunua pale Kisutu ikiwa mpya kabisa mnamo Julai 2008, na haijawahi kusumbua na ndiyo ninayotumia kuandika ujumbe huu. Sifa za kiufundi za hii laptop ni hizi:-
-Processor: AMD Turion 64x2 Mobile Technology TL 60, 2.00 GHz
-Memory 3GB
-32 Bit System
- Ina webcam
-Ina mic na speaker
-Ina Wireless Network card
-Ina Internal network card
-250 GB Hard Disk
-Uzito ni 2.9 kg
- Ina 5 in 1 Card Reader
- Ina Firewire
- 3 USB Ports
-Ina remote controller
-Screen yake ni inchi 14
-DVD RW Drive
Ni laptop imara kwa vigezo vyangu, kwa sababu huwa nashinda nayo maporini kwenye vumbi, kwa mujibu wa kazi zangu. Zipo za namna hiyo hiyo zilizoboreshwa, zenye vigezo vingi na bora kuliko nilivyotaja hapo juu, na zinapatikana kwa urahisi kwenye maduka ya kompyuta, Kisutu ama mengine yaliyojaa mtaa wa Samora. Cha muhimu, uwe na muda wa kutosha kuzunguka maduka mengi iwezekanavyo, ili upate bei elekezi na vigezo linganifu kwa kadri ya mahitaji yako.
Natumaini maelezo yangu yatasaidia 'kidogo' kukupa mwanga.
Kwenye red: nina HP na Toshiba zote ni used ni zuri sana....Kama utahitaji unaweza kuni PM (private Message)
Kwenye red: nina HP na Toshiba zote ni used ni zuri sana....Kama utahitaji unaweza kuni PM (private Message)