Kwa kweli sikushauri utumie Egypt air. Niliitumia back in July from London to Dar kupitia Cairo. Kwanza jamaa hawazingatii muda hata kidogo. Tulianza kupoteza muda London kwani ndege ilichelewa kwa masaa mawili. Kwa kuwa tulikuwa tunaunganisha ndege pale Cairo niliwauliza kama tutawahi na walinihakikishia kuwa tutawahi na walinicheck-in mpaka sector ya Cairo-Dar. Cha ajabu tulipofika Cairo saa sita usiku (Cairo time) tulikuta ndege imeshaondoka kuelekea Dar. Tuliambia kuwa tutawekwa kwenye ndege inayofuata ambayo itaondoka masa 24 baadae. Haya maneno tulikuwa tunaambiwa kwa dharau kubwa tu na wawakilishi wa Egypt air pale Cairo. Mpaka tunapelekwa hotelini ilikuwa saa 12 asubuhi. Kwa kuwa nilikuwa na mtot mdogo wa miaka 2, nilipata taabu sana. Toka siku hiyo nimeapa kuwa sitatumia huduma za Egypt air tena.
Mkuu Shakazulu,
Airline yoyote inaweza kuchelewa kutokana na matatizo mbali mbali hata KLM, Swissair, BA, Kenya Airways na hata hao Quatar wanaweza kuchelewa tu. Na kuchelewa kwa ndege not neccessarily uwe ni uzembe wa airline, kuna hali mbaya ya hewa, kuna uwanja kufungwa kwa sababu ya accident n.k. Nimesafiri na Egypt Air karibu mara nne lakini sijawahi kukutwa na hayo uliyoyaeleza.
Tiba.
Karibu tena Bongo.Wazee Heshima Mbele!
Ile safari ndio imekamilika kwa kweli na ni majaaliwa ya Mwenyezi Mungu kila kitu kimeenda shwari na sasa nimerejea kwenye kiota changu hapa bongo, salama bin salimini. Nimetumia hudma za Qatar na ukweli lazma usemwe kuwa sikupatwa na masaibu makubwa.
Nashukuru kuwa ushauri wenu ulizingatiwa na hapan' shaka tutaendelea kupeana mikakati ya kimaisha kwa kuwa naamini JF kuna vichwa lukuki na watu wenye xperiens ndefu yenye kuhitajika, ukiondoa wakorofi wachache.
In'challah Mwenyezi Mungu atawajaalia nyote.
Masalama.
Wazee Heshima Mbele!