Habari wana JF..
Naomba msaada kwenye simu yangu....
Ijumaa Iliyopita Nilijiunga Kifurushi cha chuo,, Ijumaa hiyo hiyoo nikajiunga kifurushi cha whatsapp ambacho kinatolewa na tigo ambacho unatumia whasapp week nzima kwa 1000/=.. Kutokana na matumizi yangu ,, MB za kifurushi cha Chuo Zimekata leo asubuhi.. Nikaamua kujiunga kifurushi cha MegaBox Ambacho Wanatoa MB 180 kwa sasa.... Jioni saa Kumi na Moja tukawa na discussion na wanafunzi wenzangu,, Nikisurf ,internet inagoma... nikajua sina MB za kutosha,, Kuangaliaa Naona Nina MB 98 lakini nikisurf still matokea yaleyale..... nikajaribu pia hata whatsapp maana kifurushincha whatsapp bado ninacho,, lakini hata whatsapp text haziendi..... nikawasha simu nikazima still no hopes... nikajaribu kuingia internet.org naona imekubali.... ikabidi niingie jf wataalamu wanisaidie...
Sijui Tatizo ni simu Yangu Au ni network ya tigo,, lakini nimewapigia customer care still no hopes...
NAOMBA MSAADA WATAALAMU