Msaada kwa wenye ujuzi wa friji

Mikanjuni

Member
Jan 27, 2012
59
14
Naomba wataalamu wa friji, namna ya kujua compressor imekwisha gasi, pia utajuaje kuwa compressor imejaa gas wakati gas inawekwa. Thanks
 
Kama gase imeisha hua linalia tuu lakini halitoi ule ubarudi wake wa ndani !! Kama ukitaka kujua kama gase imejaaa hapo huu kabisa kwa pembeni kuna vyuma viwili virefu kiasi kama vidole hicho kimoja kina kidude kama kifuniko!! Hicho kingine kimezibwa!! Hicho chenye kifuniko kishike kana kinaubaridi mkuu hiyo ni full gase!! Na sayansi ingine kama ukilizima pigapiga hiyo compressor na kitu chenye uzito kama kixhuma vile!! Sikiliza mlio utakao toka kama ni sauti kubwa nyepesi hapo gase kwisha kama mlio mzito baba gase ipo!! Fanya hivyo lete mrejesho!!
 
Swali la ziada. Friji linayo sehemu mbili :
- sehemu ya juu ambayo inagandisha, freezer.
-sehemu ya chini ambayo inayo baridi wastani.
Nini tatizo inapelekea sehemu ya juu(freezer) kutogandisha na sehemu ya chini kuwa na baridi Kali kuliko kawaida hadi kufanya barafu?
 
Asante kwa kunifungua macho na utaalamu. Nitarudisha mrejesho jioni sasa nipo Job muda wa Magufuli huu
 
Mkuu hapo ndani kuna adjust volume ya speed gerji inategemea umeweka ngapi kuna sehemu volume inaanza moja hadi sita au tano! Hapo inategemea wewe umeweka volume ngapi ndo maana inagandisha zaidi chini kuliko juu!!
 
Fundi ndiyo anaweza kukuchekia uwepo wa gas kwenye system au la.
Hiyo gas ina kuwa na liquid na pressure, compressor inapokuwa inafanya kazi hupamp hiyo gas kutoka lower side of the unit kwenda higher side.
Kwenye compressor kuna pump ambayo imefungwa juu ya springs. Utakapoigonga kama mchangiaji mmoja alivyoshauri lengo ni kuwa uweze ku feel myumbo wa liquid gas iliyoko kwenye low side (ndani ya tungi la compressor)

Ikiwa utatekeleza ushauri huo tegemea kufelishwa na Springs zinazoibeba pump.
Maana pump itanesanesa juu ya Springs mithili ya myumbo wa liquid gas, na huo ndio utakuwa mwanzo wa ugomvi na fundi wako.

Mwamini fundi wako. Pia uwe na akiba ya ufahamu kuwa fridge ni complex unit.
Ina consist three if not four independent systems.
1. Mechanical
2. Electrical
3. Piping
4. filtration

Moja kati ya hivyo inaweza kumfelisha fundi wa refrigerator kukutengenezea refrigerator yako.

Mpe ushirikiano anaouhitaji.
Usije leta mambo ya kujifunzia ku generate logics kanakwamba fundi anakuibia.
 
Naomba wataalamu wa friji, namna ya kujua compressor imekwisha gasi, pia utajuaje kuwa compressor imejaa gas wakati gas inawekwa. Thanks
Hilo la kuisha gas utaona frij haipozi au inachukua muda kupoza au inapoza juu chini haipozi.
Kuhusu kujaa hilo sina uzoefu nalo
 
Kwenye zile coil,coil moja imevimba kama kamtungi hivi na nimekuta inavunjisha matone ya maji...na fridge imeacha kupooza..tatizo ni nini fundi
 
Mkuu hapo ndani kuna adjust volume ya speed gerji inategemea umeweka ngapi kuna sehemu volume inaanza moja hadi sita au tano! Hapo inategemea wewe umeweka volume ngapi ndo maana inagandisha zaidi chini kuliko juu!!
nimeweka 5 kutoka 7, nasubiri kuona kama itapooza chini maana inagandisha juu ila chini hakuna hata ubaridi
 
Back
Top Bottom