Fundi ndiyo anaweza kukuchekia uwepo wa gas kwenye system au la.
Hiyo gas ina kuwa na liquid na pressure, compressor inapokuwa inafanya kazi hupamp hiyo gas kutoka lower side of the unit kwenda higher side.
Kwenye compressor kuna pump ambayo imefungwa juu ya springs. Utakapoigonga kama mchangiaji mmoja alivyoshauri lengo ni kuwa uweze ku feel myumbo wa liquid gas iliyoko kwenye low side (ndani ya tungi la compressor)
Ikiwa utatekeleza ushauri huo tegemea kufelishwa na Springs zinazoibeba pump.
Maana pump itanesanesa juu ya Springs mithili ya myumbo wa liquid gas, na huo ndio utakuwa mwanzo wa ugomvi na fundi wako.
Mwamini fundi wako. Pia uwe na akiba ya ufahamu kuwa fridge ni complex unit.
Ina consist three if not four independent systems.
1. Mechanical
2. Electrical
3. Piping
4. filtration
Moja kati ya hivyo inaweza kumfelisha fundi wa refrigerator kukutengenezea refrigerator yako.
Mpe ushirikiano anaouhitaji.
Usije leta mambo ya kujifunzia ku generate logics kanakwamba fundi anakuibia.