Msaada kwa wataalam wa kodi kuhusu Wthholding Tax

Wambandwa

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
2,249
831
Waungwana wana JF, nawapa salaam,

Ama baada ya salaam, naombeni busara kutoka kwa wabobezi wa maswala ya kodi (kama nilivyoonyesha kwenye kichwa cha habari hapo juu).

Naishi kwenye nyumba ya kupanga na nimekaa kwenye nyumba hii tangu 2008. Mwenye nyumba amekuwa na tabia ya kupandisha kodi kila baada ya miaka miwili jambo ambalo limenifanya niwe kwenye wakati mgumu.

SWALI LANGU: Hivi hii sheria ya withholding tax inawahusu wapangishaji nyumba za biashara na SI nyumba za kuishi?

Naombeni msaada wa kitaalamu kwa mwenye uelewa zaidi

Nawasilisha ombi.
 
Withholding tax ni kodi unayotakiwa kulipa TRA 10% ya fedha unazomlipa mwenye nyumba.Ni wajibu wa mpangaji na si mpangishaji kulipa withholding tax.
 
Withholding tax ni kodi unayotakiwa kulipa TRA 10% ya fedha unazomlipa mwenye nyumba.Ni wajibu wa mpangaji na si mpangishaji kulipa withholding tax.
Hiyo inakuwa added kwenye hela ya mwenye nyumba au inapunguzwa?
Kwa mfano,
Pango ni Tshs 100,000/=
10% ni Tshs 10,000/=
Sasa
1. Jumla ya malipo itakuwa ni 110,000/- kwamba 100,000/= ni ya mwenye nyumba na 10,000/- ni withholding tax..??
2. Jumla ya malipo itakuwa ni 100,000/- kwamba 90,000/= ni ya mwenye nyumba na 10,000/- ni withholding tax..??
 
Inapunguzwa kwenye kodi kuu kama tunavyolipia pango la ofisi. Ila mashaka yangu ni kama hata nyumba za kuishi tunapaswa ku with old hiii tax!
 
Withholding tax ni kodi unayotakiwa kulipa TRA 10% ya fedha unazomlipa mwenye nyumba.Ni wajibu wa mpangaji na si mpangishaji kulipa withholding tax.

Asante mkuu, nilipeleka swala hili serikali za mitaa, inaonekana hawajui sheria, kwanza walinifokea kwamba najifanya najua wakati sijui kitu. Wanasema mwenye nyumba (aliitwa pia) analipa kodi ya jengo, nikasema wanachanganya mambo kama kweli analipa kodi alete namba yake y mlipa kodi (TIN). Nikaonekana mkorofi nikafukuzwa na mwenye nymba kanipa notisi ambayo eti nilipe hiyo miezi ya notice.
 
Hiyo Withholding tax kwenye kodi ya nyumba ni kwa makumpuni tu haihusu watu binafsi. ikiwa kampuni imepanga haina budi kukata hii kodi (10%) kabla ya kumlipa mwenye nyumba.
 
Asante mkuu, nilipeleka swala hili serikali za mitaa, inaonekana hawajui sheria, kwanza walinifokea kwamba najifanya najua wakati sijui kitu. Wanasema mwenye nyumba (aliitwa pia) analipa kodi ya jengo, nikasema wanachanganya mambo kama kweli analipa kodi alete namba yake y mlipa kodi (TIN). Nikaonekana mkorofi nikafukuzwa na mwenye nymba kanipa notisi ambayo eti nilipe hiyo miezi ya notice.

Kodi ya jengo ni tofauti na withholding tax.
 
Hiyo Withholding tax kwenye kodi ya nyumba ni kwa makumpuni tu haihusu watu binafsi.

Unanifanya nihisi na wewe unapangisha manyumba Ila, nime google TRA website nikakutana na hiki:

Withholding tax
Introduction:

Withholding tax is the amount of tax retained by one person when making payments to another person in respect of goods supplied or services rendered by the payee. A person receiving or entitled to receive a payment from which income tax is required to be withheld is a withholdee while a person required to withhold income tax from a payment made to a withholdee is referred to as the Withholding Agent.

Payment subject to Withholding Tax.

Withholding tax applies to specific payments including payment that is to be included in calculating the chargeable income of an employee from the employment, payment of investment return including dividend, interest, natural resource payment, rent or royalty, payment in respect to service fee and contract payments and payment in respect to supply of goods to the government and its institutions.

Nimeweka bold na italics kuweka msisitizo. Kusingekuwa na mvua nje ningekwenda TRA hapo ni jirani kwangu nipewe mwongozo.
 
Waungwana wana JF, nawapa salaam,

Ama baada ya salaam, naombeni busara kutoka kwa wabobezi wa maswala ya kodi (kama nilivyoonyesha kwenye kichwa cha habari hapo juu).

Naishi kwenye nyumba ya kupanga na nimekaa kwenye nyumba hii tangu 2008. Mwenye nyumba amekuwa na tabia ya kupandisha kodi kila baada ya miaka miwili jambo ambalo limenifanya niwe kwenye wakati mgumu.

SWALI LANGU: Hivi hii sheria ya withholding tax inawahusu wapangishaji nyumba za biashara na SI nyumba za kuishi?

Naombeni msaada wa kitaalamu kwa mwenye uelewa zaidi

Nawasilisha ombi.
Mkuu, WHT kwa sasa kwenye nyumba zetu huku za uswahilini sheria haitubani ukiondoa wale wa apartment registered na nyumba zinazopangishwa kama maofisi, wao wanapaswa kulipa WHT tena 10% na wakionyesha mikataba yao ofisi ya TRA, ila naona kuna utaratibu unaandaliwa wa kuweza watu kuja kulipia:
 
Back
Top Bottom