Msaada kwa wanaojua masuala ya computer

davetz28

JF-Expert Member
Dec 17, 2017
543
617
Habari za asubuhi wanajamii wenzangu,poleni na hongereni kwa kazi za kujitafutia ridhiki za kila siku.
Nipo hapa leo kuomba msaada kwenu kama mada nilivyoitambulisha hapo juu.

Laptop yangu ilizima ghafla na baada ya kumpelekea fundi aliniambia tatizo lipo kwenye mother body ya laptop hiyo na aliniambia ili ifanye kazi ni lazima ninunie mother body nyingine.

Swali langu ni ie ufanisi wa komputa hiyo baada ya kubadilishwa utakuwa sawa au kuna matatizo gani mara nyingi komputa zikibadilishwa huibuka?

Je inaweza kudumu kwa muda mrefu au nianze tu mchakato wa kutafuta mpya?

Nahitaji mchango wenu wa mawazo,sielewi maana ni kama bado mpya.

Asante sana.
 
Unaposema Computer haiwaki unamaanisha nini?

Je ukibonyeza On inaonyesha moto umeingia ila kioo hakionyeshi kitu?(Booting)

Au Ukibonyeza On moto hauingii kabisa kwenye Computer? (Doesn't Power On)

Kama sio motherboard kupiga shot basi hakuna sababu ya motherboard kufa tu. Lazima kuna vifaa vimeharibika.

Je amekagua Ram,HDD, CPU,Bios Chip, Power Supply, akakuta zote ni nzima?

Kma jibu ni ndio basi jaribu kupeleka kwa watu waliosomea zaidi electronics wanaweza kukusaidia (Mafundi computer wengi hawajabobea kwenye Electronics)

Kama jibu ni hapana basi akague vizurii fundi hata mwingine anaweza kuona tatizo.

Ila kama motherboard imekufa basi kanunue laptop mpya tu ili kuepuka usumbufu na ghalama. Kitu kikishaenda kwa fundi basi kinabaki Reckless
 
Laptop nadhubuti haiwezi kufa tu kirahisi namna hiyo, ja uliinunua mpya au iliyotumika? Na imeitumia kwa muda gani na je ilikuwa inasumbua kabla ya hapo, kama ilikuwa inasumbua ni tatizo gani lilikuwa linajitokeza mara kwa nara?
 
Nimetumia kama mwaka mmoja hivi,kabla haikuwa kusumbua,fundi anasema huenda maji yaliingia maana siku ya tukio nilimwachia kijana wangu alikuwa akicheza game sasa sijui kilichoendelea,siku ya pili nawasha haikuwaka.
 
Unaposema Computer haiwaki unamaanisha nini??
Je ukibonyeza On inaonyesha moto umeingia ila kioo hakionyeshi kitu??(Booting)...
Asante kaka,mimi sifahamu sana kukagua hivyo ulivyovitaja,ila power ilikuwa sawa,hata nilipimpelekea fundi wakati anapima alisema kuna sehemu moto unaenda lakini upande wa pili haipokei sasa aliniambia inaweza kutengenezeka na aliniambia gharama ni shilingi 180000,vifaa na fundi.

Nikampelekea fundi mwingine naye kwa kiasi fulani aliniambia inaweza kutengeneza na gharama ni 150000.

Niliona pesa nyingi na hivyo nikaamua kuiweka tu ndani lakini nikiumia kwa sababu kuiweka ndani means kuiua kabisa. Hii ndio nikaona niombe ushauri ili niangalie value for money
 
Laptop nadhubuti haiwezi kufa tu kirahisi namna hiyo, ja uliinunua mpya au iliyotumika? Na imeitumia kwa muda gani na je ilikuwa inasumbua kabla ya hapo, kama ilikuwa inasumbua ni tatizo gani lilikuwa linajitokeza mara kwa nara?
Nilinunua mpya kabisa tena dukani
 
Nunua laptop nyingine tu ndugu yangu, gharama ya kuifanyia matengenezo ikiwemo kununua motherboard mpya hadi infanye tena kazi ni kubwa kuliko kununua iliyotumika.

Hata mimi nina HP ilizimika ghafla nikazunguka nayo kwa mafundi wa kila aina imeshindikana. Iko vizuri tu kimuonekano lakini haifanyi kazi.
 
Habari za asubuhi wanajamii wenzangu,poleni na hongereni kwa kazi za kujitafutia ridhiki za kila siku.
Nipo hapa leo kuomba msaada kwenu kama mada nilivyoitambulisha hapo juu.

Laptop yangu ilizima ghafla na baada ya kumpelekea fundi aliniambia tatizo lipo kwenye mother body ya laptop hiyo na aliniambia ili ifanye kazi ni lazima ninunie mother body nyingine.

Swali langu ni ie ufanisi wa komputa hiyo baada ya kubadilishwa utakuwa sawa au kuna matatizo gani mara nyingi komputa zikibadilishwa huibuka?

Je inaweza kudumu kwa muda mrefu au nianze tu mchakato wa kutafuta mpya?

Nahitaji mchango wenu wa mawazo,sielewi maana ni kama bado mpya.

Asante sana.
Mkuu specs zake zipoje? 180k itategemea na uzuri wa hio laptop.
 
Back
Top Bottom