Msaada kwa rafiki yoyote wa dhati

1995_No_Ku_Fake

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2026
Posts
1,323
Reaction score
2,832
WAKUU NAOMBA MNISIKILIZE KIDOGO πŸ™

Sijui hata nianzie wapi kusema, lakini nimeamua kuandika hapa kwa sababu kwa sasa nimefika sehemu ambayo nahitaji msaada wa mtu mwenye moyo wa kusaidia.

Kwa siku hizi nimekuwa napitia hali ngumu sana. Mawazo yamekuwa mengi, mambo yamekwama na kwa sasa sina uwezo wa kujinasua mwenyewe kama nilivyokuwa nikitamani. Sijaandika huu uzi kwa kutaka huruma wala kutafuta umaarufu JF, nimeandika kwa sababu kweli nimekwama.

Kama kuna mtu anaweza kunisaidia kwa namna yoyoteβ€”iwe ni chakula, kiasi kidogo cha pesa, kazi ya kufanya, connection ya kazi, au hata ushauri wa kunipa mwelekeoβ€”nitashukuru sana. πŸ™

Sihitaji mtu anipe maisha; nahitaji msaada wa kunivusha kwenye hiki kipindi ili niweze kusimama tena.

Kama unaweza kusaidia, tafadhali DM yangu iko wazi. Na kama huwezi, hata dua yako na neno la kunitia moyo vina maana kwangu.

Mungu awabariki wote watakaogusa maisha yangu kwa namna yoyote. 🀲

Nimeandika kwa unyenyekevu mkubwa. πŸ™
 
Mkuu juzi ulifungua uzi kuna mtu akakuandikia namba umtafute. Mliishia wapi?
Hawa watu wa humu wanaombaga msaada ila wana conditions zao, yan kuna vigezo vyao wanakupa unatakiwa kuvi meet ndio uwasaidie. No wonder no one bothers.
NB
Sijaandika kwa ubaya ila naamini kuna watakao kuwa wamekutana na ishu kama hiz. Mimi nishakutana nazo kadhaa. Na niwe mkweli wala sionagi huruma tena kwa watu wa nyuzi kama hizi
 
Kaka Fanton habari yako.... Naomba nguruwe mwenye mimba.... Nikichukua asiye nayo siwezi mkuu πŸ˜†
 
Humu kuna watu wa hovyo sana, nishawah kusaidia jamaa kumbe wema kumanyoko!
 
Kila siku jmaa anatia huruma yeye tu, kuna mwenzie mpaka akabadilishaga na jina mana walimsaidia ikapita kipindi fulan akarud ten kuomba na maneno alitumia yaleyale ya mara ya kwanza.
 
Asante Sana
 
Wakati ambao unatumia utashi wa ujana wako kwenye hii safari ya maisha,Wapo wanaopifia kweli.

Kijana niliwahi kukwambia
(Acha kujisndekeza utabakwa.)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…