msaada kwa mwenye kujua hili kuhusu malaria

msaada kwa mwenye kujua hili kuhusu malaria

aka2030

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
2,674
Reaction score
3,741
nimekuwa na tatizo moja sasa nimekuwa naumwa maralia mara kwa mara.Yani kupita mwezi bila kuumwa inakuwa ni ajabu sana,na cha zaidi ni malaria nshapima vyote vipimo muhimui nipo sawa. sasa naomba kwa mtu mwenye uelewa shida itakuwa ni nini maana inanikwamisha muda mwingine kufanya mambo mengine.kama unajua dozi ama daktari wa kumuona naomba unambie na hospitali pia nzuri kwa vipimo
 
Pole Sana Mimi Mwenyewe Nilishawahi Kutokewa Na Hali Hiyo Ya Kuugua Malaria Kila Mwezi Baada Ya Kugundua Hilo Nilimweleza Doctor Na Akaniandikia Dozi Ya Quinine Nilvyomaliza Kuitumia Ckuona Tena Malaria Karibu Mwaka Wa Pili Sasa Nakushauri Nenda Hosptal Mweleze Doktor Hilo Tatzo Mweleze Na Dawa Ulizowahi Kutumia Yeye Atajua Namna Ya Kukusaidia. Kuhusu Hospitali Nzuri Cjajua Uko Wapi Ila Nenda Hospital Za Kawaida Za Serikali Mm Nlienda Mgmn Hospitali.
 
Pole Sana Mimi Mwenyewe Nilishawahi Kutokewa Na Hali Hiyo Ya Kuugua Malaria Kila Mwezi Baada Ya Kugundua Hilo Nilimweleza Doctor Na Akaniandikia Dozi Ya Quinine Nilvyomaliza Kuitumia Ckuona Tena Malaria Karibu Mwaka Wa Pili Sasa Nakushauri Nenda Hosptal Mweleze Doktor Hilo Tatzo Mweleze Na Dawa Ulizowahi Kutumia Yeye Atajua Namna Ya Kukusaidia. Ugua Pole.

Alikuandikia sindano ama vidonge?
 
Sema huwa unatumia dawa gani. Dawa kama sp amodiaquine hazitibu malaria cha kufanya nenda hospital uandikiwe dawa. Na epuka kutumia dawa bila kuandikiwa na Dr
 
mmmh kupita mwezi bila kuugua inakuwa ajabu sana

ukiumwa na mbu anophelesi hadi unaanza kupata dalili za kwanza za malaria ni kuanzia siku 7 hadi 30 tangu ulipo umwa

na kama unameza dawa then mwezi unaokuja unaumwa tena
nachelea kusema huko unapotibiwa either wana ku mis diagnose
au unaishi kwenye chumba unachofuga mbu tena anophelesi

au hauendi hosptital unajimezea mezea dawa kila ukihisi dalili kama za malaria

basi kapime tena kwenye hospitali zinaoeleweka : ukikutwa unayo
kanunue dawa inayoitwa mefaquine
vidonge vipo vinne
unameza 2x1 kwa siku mbili
then uje kutoa feedback hapa
 
nshatumia metakelfini,mseto,co-malafin na duo cotexin lakini wapi unakuta natulia miki kazaahali ilakuwa ile ile mara ya kwanza nilikuwa nahisi may be msuli wa chuo lakini namuda nimemaliza mambo yale yale
 
aisee hili tatizo hata mimi linanitatizo na hii hali imeanza si muda sana na pia sio mimi tu hata kaka yangu pia na yeye huwa haiwezi pita muda lazima atanilalamikia anamaralia nashindwa jua shida ni nini maanakama net natumia,dawa yambu napulizia,kuna kipindi mpaka ile ya kupaka nilikuwa napaka pia
 
Poleni cha msingi pima malaria, pia pima typhoid ili kama ni homa za aina nyingine ijulikane. Malafin, duo cotexin na metakelfin zimekuwa hazitibu wengi tu, ukinywa ukimaliza wk 2 waweza sikia homa palepale. Co artem nayo imeishapungua baadhi haiwatibu, usikimbilie quinine ni dawa ya mwisho. Kuna dawa zinaitwa artequine ni nzuri na zinatibu vizuri tu. Cha msingi nenda hospitali pima mweleze dr usugu wa dawa ulizotumia akuandikie dawa ingine. Kuna watu kwa asili kinga sio juu jitahidi kutumia net na pia pakaa repellants zinauzwa cheap ni muhimu.
 
nshatumia metakelfini,mseto,co-malafin na duo cotexin lakini wapi unakuta natulia miki kazaahali ilakuwa ile ile mara ya kwanza nilikuwa nahisi may be msuli wa chuo lakini namuda nimemaliza mambo yale yale

Malafin haitibu malaria, we hzo dawa unaandikiwa na nani au unajimezea tu??
 
nimekuwa na tatizo moja sasa nimekuwa naumwa maralia mara kwa mara.Yani kupita mwezi bila kuumwa inakuwa ni ajabu sana,na cha zaidi ni malaria nshapima vyote vipimo muhimui nipo sawa. sasa naomba kwa mtu mwenye uelewa shida itakuwa ni nini maana inanikwamisha muda mwingine kufanya mambo mengine.kama unajua dozi ama daktari wa kumuona naomba unambie na hospitali pia nzuri kwa vipimo

Ushajua ugonjwa ni malaria bac umeshakua DR sasa c unywe dawa,dawa kiboko cha malaria ni Quinine
 
nshatumia metakelfini,mseto,co-malafin na duo cotexin lakini wapi unakuta natulia miki kazaahali ilakuwa ile ile mara ya kwanza nilikuwa nahisi may be msuli wa chuo lakini namuda nimemaliza mambo yale yale

nna mashaka na sehemu unazotibiwa
 
nimekuwa na tatizo moja sasa nimekuwa naumwa maralia mara kwa mara.Yani kupita mwezi bila kuumwa inakuwa ni ajabu sana,na cha zaidi ni malaria nshapima vyote vipimo muhimui nipo sawa. sasa naomba kwa mtu mwenye uelewa shida itakuwa ni nini maana inanikwamisha muda mwingine kufanya mambo mengine.kama unajua dozi ama daktari wa kumuona naomba unambie na hospitali pia nzuri kwa vipimo
Pole sana. Kama alivyosema mchangia mmoja mimi nadhani quinine inaweza kuwa dawa nzuri kwako lakini usinywe kienyeji bila kumwona daktari. Pengine vijidudu vya malaria vitakuwa vinakimbilia kwenye ini kujificha kila unapomeza dawa, ndio maana nimesema quinine inaweza kuwa chaguo zuri. Halafu kuna dawa nyingine zinaitwa
primaquine. Hizi ni special kukabiliana na vijidudu vinavyojificha kwenye ini na inabidi umeze dozi ndogo kwa siku 15. Jambo la muhumu ni USITUMIE DAWA BILA KUANDIKIWA NA DAKTARI.
 
Back
Top Bottom