Msaada kwa mwanangu

713

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2018
Posts
354
Reaction score
778
Habari za jioni wana jukwa.

Kwa muda sasa kuna hali inamtokea mwanangu ila sijui ni ugonjwa au ni kitu gani. Akiwa na mwaka moja kama mnavojua watoto alikuwa anacheza katika sehemu ya hatari, nilishikwa na hofu maana ni kwenye ngazi.

Basi nikamfokea, ila baada ya hapo ndiyo tatizo likaanza. Alikuwa analia kama anakakamaa hivi, pumzi hazitoki yaani anabaki kimya tu. Nilimchukua kwa uwoga na kumuweka kifuani na kumbembeleza.

Leo akiwa na umri wa miaka 2 na miezi 3 imetokea tena, safari hii akiwa na mama yake wametoka dukani karibu na nyumbani akataka abebwe mama yake akampiga kibao kidogo akaanza kulia na kujitupa chini na kuanza hali kama ya mwanzo kama anakaukia hivi. Mama yake alilia sana na badaye alikaa sawa.

Naomba ushauri kwa madakatari na hata ambao watoto wao wanahali kama hiyo. Shida ni nini au nifanyeje mwanangu asiwe na hali hiyo? Nahofia akifika umri wa kusoma itakuwaje huko shuleni au kwa ambaye hamjui ikimtokea itakuwaje?

Naombeni msaada wenu wanajukwaa.
 
Asante ndugu ila degedege akilia tu au kufokewa
 

Hizo ni dalili za

Degedege (seizure)

Kifafa (epilepsy)

Mpeleke haraka MOI kwa mabingwa wa mifumo ya fahamu akafanyiwe vipimo CT Scan au MRI ya kichwa kujua sababu

The early the better
 
Pole naona kama ni degedege sasa kabla haijakomaa ikazaa kifafa ebu mjarbu hii dawa chukua majan ya mbaazi na vitunguu saum uvitwange pampja loweka uwe unampa vjko 3..4 ndan ya wki alafu uwe unampakaza kitunguu saum mwli mzima ikiendelea baada ya wki 2 tena urudie hyo dawa kumpa Mungu atamsaidia atapona
 

Asante sana mungu akubariki
 
Hizo ni dalili za

Degedege (seizure)

Kifafa (epilepsy)

Mpeleke haraka MOI kwa mabingwa wa mifumo ya fahamu akafanyiwe vipimo CT Scan au MRI ya kichwa kujua sababu

The early the better

Asante sana ubarikiwe ndugu ila samahan naweza jua gharama ya hivo vipimo au kama vipo kwenye bima niweze kujipanga
 
Mkuu mpeleke hospitalini mapema achana na story za mavi ya tembo au vitunguu saumu vitakuchelewesha. Ishu ya ubongo sio ya kufanyiwa mjaribio. Mimi mwanangu alikua na shida hio nilimpeleka pale muhimbilo kuna daktari anaitwa Dkt Bensoy..namba sina ila nikiitafuta nitaipata. Aliniandikiwa dawa ambayo nilinunua na shida iliisha.
 
Reactions: 713


1. Mtoto anaomba abebwe anapigwa kibao???????

2. Mtoto wenu ana hasira kali sana.
 
msirudie kumzibua mtoto wenu kabla hajapata tiba, muogesheni kwa maji yenye mchanganyiko wa mchaichai(yalihofikichwa) na vitunguu swaumu vilivyosagwa vikachanganywa na maji bila kutumia sabuni hasa nyakati za usiku,hiyo ni tiba ya kienyeji.
 
1. Mtoto anaomba abebwe anapigwa kibao???????

2. Mtoto wenu ana hasira kali sana.

Kuna mda inatokea tu kama mzazi unaona mwanao anafanya kitu cha hatari au una mtani kama hiyo ya mama ake alikuwa ana mtania tu kuna kupiga na kumgusa nikama alimgusa tu jaman mtto wa miaka 2 utampiga wapi
 
msirudie kumzibua mtoto wenu kabla hajapata tiba, muogesheni kwa maji yenye mchanganyiko wa mchaichai(yalihofikichwa) na vitunguu swaumu vilivyosagwa vikachanganywa na maji bila kutumia sabuni hasa nyakati za usiku,hiyo ni tiba ya kienyeji.

Asante ndugu nitafanya lolote kwa mwanangu jaman mradi apone
 

Asante kaka Mimi nip tayari kwa lolote msaada wa namba ukipata
 
Nakumbuka mdogo wetu wa mwisho nae alikuwa analia ana kakamaa.
Alikuwa akikakamaa tunanyamaza wote kimya kwa hofu.

Ila baadae hio hali haikumtokea tena hadi leo yuko sekondari.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kaka Mimi nip tayari kwa lolote msaada wa namba ukipata
Dr Bensoy
0699254400. Mpigie mwambie umepewa namba na mama maiko wa dodoma atakumbuka.
 
Nakumbuka mdogo wetu wa mwisho nae alikuwa analia ana kakamaa.
Alikuwa akikakamaa tunanyamaza wote kimya kwa hofu.

Ila baadae hio hali haikumtokea tena hadi leo yuko sekondari.


Sent using Jamii Forums mobile app
Aise kuna mdg Wang nae anashid hiyo hiyo had saiz yan asipo meza tu vidonge vyake vinaitwa( phemabebiton) nazan lazma aataanza kukaamaaa mwili yan ile hali inatisha Sana'a cjuh mpk dawa gan utumie itaacha kabis bila kunywa kila cku vidonge ivyo;!
 
Reactions: 713
Asante sana ubarikiwe ndugu ila samahan naweza jua gharama ya hivo vipimo au kama vipo kwenye bima niweze kujipanga

Bima ina cover mkuu

Usibet kwenye maisha ya mwanao na mavi ya sungura mara sijui majani ya mpera

Nenda hospitali mkuu
 
Reactions: 713
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…