God bless you a lot
Kama walivyokwambia wadau, social media achana nazo baada ya kupata mawazo uliyohitaji. Usikatishwe tamaa na baadhi ya comments.
Tumia bando yako kwa ajili ya kutafuta materials mbalimbali hasa yale mambo unayoyakosa katika vitabu ulivyonavyo yanayohusiana na masomo yako PCM yaliyo katika syllabus.
Hakikisha unakuwa na past papers za kutosha bila kusahau za NECTA. Uwapo darasani jitahidi uelewe, usione haya kuuliza kwa walimu au wenzako pale ulipoachwa. Tumia past papers kama kioo kwa kila topic uliyo cover, fanya maswali yakutosha.
Discussion na wenzako ni ya muhimu sana, vitabu vyako vitakuwa msaada sana pale utakaposhirikiana na wenzako, usiwe mchoyo. Hakikisha unakuwa na discussion ambayo ni productive, achana na discussion ambazo sehemu kubwa ni stories na utani.
Heshimu muda kupumzika. Weka ratiba yako vizuri kbs. Kama ni mtu wa msuli, kamdamiza hasa, tenga na muda wa kupumzika na some sort of leisure time kidogo mfano kuangalia mpira au listening to musics. Mambo ya mademu kuwa makini kwa sasa, muda ni mchache sana, ukijichanganya utapata chombo kitakushika akili badala ya kuwaza ma integration na differentiation, maclomplex unawaza appointment. Hizo mambo zipo utazikuta.
Last but not least, mwombe sana Mwenyezi Mungu akujaalie afya, ari ya kusoma, na mwongozo katika masomo yako.
Nakutakia kila la heri katika masomo yako. Usisahau kuweka pembeni social media baada ya kupata feedback uliyoihitaji. Humu unaweza kukatishwa tamaa au ukajengwa. Kuwa makini.