Msaada: Kwa laki na nusu naweza kufuga kuku wa aina ipi?

mathsjery

JF-Expert Member
Sep 26, 2015
2,241
1,794
Mimi ni mwanachuo mwaka wa kwanza ila natamani nifanye ufugaji huko Mwanza nyumbani ni Bugarika. Nauliza kwa laki na nusu naweza kufuga kuku wa aina ipi na nitapata faida gani, msaada jamani?!
 
Fuga kuku wa kienyeji ambao ni rahisi kuwatunza,lkn mimi ninakushauri ununue matetea 9 (Tshs.90,000/),na jogoo mkubwa mmoja(Tshs.20,000),halafu pesa inayobaki tengenezea box lenye ukubwa wa 2m za ukubwa kwaajili ya kukusanyia vifaranga kwa kuwanyang'anya mama zao kila wanapofikisha wiki mbili au tatu tangu kutotolewa,yaani ninakwambia ndani ya mwaka mmoja utakuwa na kundi kubwa la kuku,mimi nimeshawahifanya hivyo nikafanikiwa sana.
 
Mkuu, kwa hiyo hivi vifaranga vitatakiwa kukaa kwenye box muda wote hata wakiwa wakubwa au? kwa mfano kwa sisi wa uswazi
 
Mkuu, kwa hiyo hivi vifaranga vitatakiwa kukaa kwenye box muda wote hata wakiwa wakubwa au? kwa mfano kwa sisi wa uswazi
Hapana mkuu,yaani wakishafikia umri ambao ni wa kujitegemea wao wenyewe basi unawatoa waendelee na maisha yao au Unawajengea banda kwaajili ya kuwafugia ndani,na hii ndo nzuri hasa km unataka kufuga kibiashara.
 
Mimi ni mwanachuo mwaka wa kwanza ila natamani nfanye ufugaji uko mwanza nyumbani ni bugarika nauliza kwa laki na nusu naweza kufuga kuku wa aina ipi na nitapata faida gani msaada jamani?!
Kwa Huo Mtaji Unatosha Kufuga Kuku Wa Kienyeji ... Ukihitaji Ushauri Zaidi Nitafute ...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom