Msaada kwa huyu mama

Shmy

Senior Member
Aug 3, 2012
148
55
Habarini za kazi wanajamii wenzangu. Kuna jambo limenigusa sana kiasi kwamba nikaona nililete humu. Napenda sana kusikiliza kipindi cha kashikashi za mtaa kupitia radio capital. Kuna mdada amemwagiwa tindikali na mumewe usoni. Lengo kubwa kupoteza uzuri wa huyo Dada ambao mume wake anadai anaulingia. Kaenda mbali zaidi anataka kummaliza kabisa huyo dada kisa Mali. Lakini hizo mali wamechuma wote na mkewe kwa kusaidiwa na baba mkwe ambaye alimruhusu binti auze kiwanja chake kilichokuwa maeneo ya malaika hoteri mwanza na kupata m200. Walifungua shule maeneo ya kahama na bado dada alikuwa na duka la jumla la nguo. Maisha yalipokaa sawa mume vituko vikaanga mara awafukuze watoto wa yule Dada kwani tayari alikutwa na watoto wawili ambao ni wa mume wa kwanza ambaye alikwisha fariki. Dada kupigwa kila kukicha mara huyo baba kutembea na wafanyakazi wa kike kwenye ile shule yake bila aibu. Dada ilibidi ampishe aanze maisha yake mwanza lakini mwanaume hakuridhika alimfatilia huko na ndiko alikotafuta vijana wakamwagia tindikali. Mwanaume alimtambia huyo dada baada ya kumchukua tena ili amtibu na sasa amemfukuza tena toka mwezi wa saba. Dada bado anamajeraha ya vidonda usoni na kifuani ameenda hospitali anatakiwa kulipa m6 ilikupata matibabu. Japo tayari amekwisha katwa nyama sehemu nyingine kuwekewa kwenye sehemu za kifua ambazo zilikuwa zimechimbika. Mume anamtafuta ammalize, watoto hata wa yule baba kawafukuza wapo kwa babu yake, hatoi msaada wowote na kila kitu mume kashikiria. Dada yupo dar es salaam ndo amekimbilia ili kupata msaada wa kisheria na matibabu pia. Nimeamua kuweka wazi hali halisi ya huyo dada. Ni mkazi wa kahama na huyo bwana amewahi kufanya kazi mgodi wa geita lakini alifukuzwa. Anayetaka kujua zaidi tumia namba hizi 0743069724 au 0713535549
 
Yaani hayo yanafanyika na serikali ipo kweli malipo ni hapa hapa duniani
 
Elimu ni tatizo kwani Hata familia yake binti imekwisha tishiwa
 
Kna mambo kama una waza negative na positive mtu hupaswi kufanya hasa kwa jamii za kiafrika.
  • Mwanamke kama mali/mtaji uliupata kwa nguvu yako bila kuchangiwa basi lolote utalofanyia liwe katika jina lako na beneficiaries wawe watoto tuu.
  • Kama mlisaidiana basi hakiki mali haina jina la mwanaume tu ila mna joint ownership.

Hii ni silaha pale unabaki mjane na ndugu wa mme wanaanza ujinga wao ama pale mmeo anapoanza kuota mabawa na kujiona high class zaidi yako.

Tukirudi kwa huyo mdada nadhani hapo ni ashikamane na baba ake wamshitaki mme na kama wana vielelezo vya kuonesha nani aliweka mtaji wa biashara zao basi wadai mali kwa kufata haki za kijinsia kuwa mme anamfuja na kumdhalilisha
 
Back
Top Bottom