Habari zenu wadau
Naomba msaada wa kiushauri kuhusu tatizo lililotokea kwenye laptop yangu.
Nina laptop aina ya lenovo.kwa muda kama mwezi mmoja display sijui imepatwa na matatizo gani.hili swala lilianza kwa kuonekana kwa msatari wa kijani kutokea na kupotea,baada ya muda ukawa hapotei tena. Hivi sasa umeongezeka mstari mwingine wa rangi nyekundu.hii inafanya idisplay mistari miwili iliyosambamba wa kijani na mwekundu.
Nimeshindwa kuelewa hili jambo lometokea kwa sababu ipi na kwa nn?.
Nimekuja kwenu nipate kujua nini tatizo na namna gani ya kulitatua.
Asantheni naomba kuwasilishaa