Msaada: Kusajili gari kutoka showroom

Msaada: Kusajili gari kutoka showroom

panyaroad

Member
Joined
Jun 9, 2014
Posts
6
Reaction score
2
Heshima kwenu wakuu, somo tajwa hapo juu lahusika.

Nadhamiria kumnunulia shemeji yenu ka usafiri kadogo aina ya passo ili kumrahisishia kwenda na kurudi kazini hasa kwa kipindi hichi ambapo yupo katika hali ya ujauzito, nimepitapita katika baadhi ya showrooms hapo mjini nikaona kagari kamoja (toyota passo) nikakapenda lakini kuulizia details kwa muhusika nikaona kuwa bado hakajapata usajili kwa maana ya namba na kadi kwakuwa muarabu alishindwa kunionyesha vitu hivyo badala yake alinijia na file lenye makaratasi mengi ikiwemo BOL na tule tukaratasi kutoka TRA twenye maandishi madogo (release order na nini sijui).

Naombeni msaada kwenu waheshimiwa kwa aliyeshawahi kununua gari show room
  1. Hichi nilichokutana nacho ni kawaida au muarabu anataka kuniingiza mjini?
  2. Kama ni kawaida je ni taratibu gani nitapaswa kufuata baada ya kununua hilo gari ili namba ya usajili na kadi ikiwemo makadirio ya gharama nitakazopaswa kulipia? Bei ya gari ni sh 7,300,000/=

Ninaomba msaada huu kwenu kwasababu:-
  1. Sina uzoefu wa kununua gari kutoka show room, nimeshawahi mara mbili kununua haya magari yaliyochoka kutoka kwa mtu ambapo baada ya mauziano hunipa mkataba na kadi ya gari ambapo nilipitisha kwa mwanasheria akanigongea mhuri kwenye mkataba nikaenda nao TRA pamoja na sh 60000+ 1% ya garama za mauziano na TIN namba
  2. Nilipita TRA pale Samora kuulizia taratibu lakini kwa bahati mbaya responce niliyopata haikuwa nzuri na ni aibu ofisi kubwa kama ile kukosa utaratibu wa kueleweka wa kuhudumia enquires za wateja.

Natanguliza shukurani
 
Kabla ya kusajili hilo gari inabidi tujue kwanza pesa za ESCROW ziko wapi..!
 
Mwarabu huyo anatakiwa akamilishe taratibu zote ikiwa ni pamoja na kusajili gari! Kama hawezi basi ni tapeli!!
 
Heshima kwenu wakuu, somo tajwa hapo juu lahusika.

Nadhamiria kumnunulia shemeji yenu ka usafiri kadogo aina ya passo ili kumrahisishia kwenda na kurudi kazini hasa kwa kipindi hichi ambapo yupo katika hali ya ujauzito, nimepitapita katika baadhi ya showrooms hapo mjini nikaona kagari kamoja (toyota passo) nikakapenda lakini kuulizia details kwa muhusika nikaona kuwa bado hakajapata usajili kwa maana ya namba na kadi kwakuwa muarabu alishindwa kunionyesha vitu hivyo badala yake alinijia na file lenye makaratasi mengi ikiwemo BOL na tule tukaratasi kutoka TRA twenye maandishi madogo (release order na nini sijui).

Naombeni msaada kwenu waheshimiwa kwa aliyeshawahi kununua gari show room
  1. Hichi nilichokutana nacho ni kawaida au muarabu anataka kuniingiza mjini?
  2. Kama ni kawaida je ni taratibu gani nitapaswa kufuata baada ya kununua hilo gari ili namba ya usajili na kadi ikiwemo makadirio ya gharama nitakazopaswa kulipia? Bei ya gari ni sh 7,300,000/=

Ninaomba msaada huu kwenu kwasababu:-
  1. Sina uzoefu wa kununua gari kutoka show room, nimeshawahi mara mbili kununua haya magari yaliyochoka kutoka kwa mtu ambapo baada ya mauziano hunipa mkataba na kadi ya gari ambapo nilipitisha kwa mwanasheria akanigongea mhuri kwenye mkataba nikaenda nao TRA pamoja na sh 60000+ 1% ya garama za mauziano na TIN namba
  2. Nilipita TRA pale Samora kuulizia taratibu lakini kwa bahati mbaya responce niliyopata haikuwa nzuri na ni aibu ofisi kubwa kama ile kukosa utaratibu wa kueleweka wa kuhudumia enquires za wateja.

Natanguliza shukurani

Usitake kujuaTechniclities.Toa hizo 7,300,000. Mwarabu atamaliza kila kitu
 
Back
Top Bottom