Msaada kupauwa kwa milunda

Msaada kupauwa kwa milunda

Andaa milunda yako kwa kuibangua maganda, urefu unaoutaka hasa kipindi cha masika.
Ukiishaiandaa, tafuta bwawa ama korongo lenye maji yasiyoweza kukauka muda chini ya mwezi mmoja.
Ipange kwenye maji izamishe kabisa muda wa mwezi mmoja halafu itoe.
Hapo sukari ya miti inayopendwa kushambuliwa na dumuzi itakuwa imeisha na haitaweza kubunguliwa na mdudu yeyote.
Mirunda hiyo itadumu zaidi ya miaka 50 bila kujali aina ya miti uliyochagua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom