Msaada kupata kazi

gambakuffu

JF-Expert Member
Jul 2, 2010
422
411
Habari wana jamvi la jf..mimi ni kijana wa miaka 29 nina stashahada ya juu ya uhasibu (ADA) kutoka CBE, nilihitimu yapata miaka 3 iliyopita yaani 2008.Kwa sasa nafanya kazi kwenye kampuni binafsi inayohusika na microcredit facilities, nina uzoefu wa miaka2 na miezi kadhaa kazini kama mhasibu..mazingira ya kazi kwa sasa si mazuri na huenda kampuni ikacollapse muda wowote kuanzia sasa na tuliomo ndani yake tukakosa ajira, hii hali mbaya ya kampuni tulishaistukia muda kidogo na kila mmoja wetu amekuwa na bidii kutafuta ajira sehemu zingine na kuna baadhi yetu washafanikiwa kung'oka.
Nawaomba wana jf msaada wenu maana ni zaidi ya mwaka sasa tangu nijihusishe na hizo harakati na nimeona ni vyema niwahusishe wana jamvi maana nina hakika kwenye wengi sikosi la maana na msaada wenu utakuwa wa manufaa sana kwangu.

Nawasilisha,

Shukrani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom