Msaada kununua umeme TANESCO Luku ( mita mpya)

Msaada kununua umeme TANESCO Luku ( mita mpya)

shaurimbaya

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2013
Posts
1,915
Reaction score
2,337
habari wadau.

ninahangaika kununua umeme muda mrefu.. kila salio inanigomea..

wadau wenye experience na hili tatizo naombeni msaada..

kila salio nalonunua naambiwa halifai.. nimejarib max malipo, mpesa,nmb mobile, kote zengwe tu etc.

je kwenye hizi mita mpya ni kiasi gani cha kuanzia kununua..
 
Hyo mita mpya hujawahi kununua Luku toka ufungiwe?kama hvyo ndivyo basi nenda kwenye vituo vya tanesco
 
Pole sana! Lkn ni vyema kupata uhakika kama mita yako ilishaingizwa ktk system ktk ofisi za TANESCO. Bila hivyo ni sawa na kusema kuwa bado hujatambulika kama mteja, na nikushauri usiendelee kujaribu kununua ktk njia hizo kwa mara ya kwanza zaidi ya vituo vya tanesco
 
Kama mita mpya na unanunua kwa mara ya kwanza...unapaswa kununulia tanesco
 
Haswaaa waliotangulia wameshakupa suluhisho, kinachotakiwa kama ndio mara ya kwanza unataka kununua umeme baada ya kufungiwa mita unatakiwa ununue kwenye kituo cha TANESCO na inatakiwa uwe na kiasi cha kutosha sijajua ni kiasi gani hasa ila cha kutosha kulipia zile unit za awali ambazo zilikuwepo wakati umefungiwa mita ambazo ni 50
 
Nenda kwa venda yeyote wa Tanesco anayeuza luku atakuingiza kwenye system
 
Ni kweli mkuu..Mimi Tanesco waliniambia baada ya kumaliza hizo 50 unit unatakiwa ununue umeme wa zaidi ya elfu 35 ndo itakubali otherwise huwezi kununua umeme..maana kwamba zile 50 units is not a bonus..unazilipia pia
 
Nenda kwa venda yeyote wa Tanesco anayeuza luku atakuingiza kwenye system

Mkuu sio rahisi kiasi hicho, hapo anachotakiwa kufanya ni kwenda ofisi ya tanesco, iliyokaribu naye, idara ya mita waifungue kwanza ndipo ataweza kununua umeme. Tena kibaya zaidi siku hizi kuna mita zao nyingine wakikuwekea zile units 50,za mwanzo usisubili ziishe kabisa mita izimike inakuwa inshu tena!! yaani inaweza ikazimika moja kwa moja isifanye kazi tena, mi kuna jilani yangu yalimkuta, hadi sasa anafuatilia mita nyingine ile ya awali haifai tena!! kisa alisubili hadi units ya mwisho, umeme ukazimika na mita ndio ikafa kabisa, na wao hawakumwambia awali, siku anaenda wanajaribu kuifungua inagoma ndio wakafuatilia ikaonekana imekufa!! ndio wakamwambia kwani wakati unawekewa hii mita hukuambiwa zikibaki kama units 5,njoo tuifungue?? hadi sasa ni pambo tu lipo ukutani, hana umeme. kosa lao linampa mteja shida.
 
habari wadau.

ninahangaika kununua umeme muda mrefu.. kila salio inanigomea..

wadau wenye experience na hili tatizo naombeni msaada..

kila salio nalonunua naambiwa halifai.. nimejarib max malipo, mpesa,nmb mobile, kote zengwe tu etc.

je kwenye hizi mita mpya ni kiasi gani cha kuanzia kununua..

Nenda ofisini kama unataka kiongeza kwa mara ya kwanza tangu ufungiwe. Si ulipewa unit 50 kama mkopo? Kama jibu ni ndiyo nenda ofisi za tanesco ni kiwango kisichopungua Tshs 35000.
 
Back
Top Bottom