1.Zipo Sheria za Mirathi za aina mbalimbali hapa Tz,, muone Wakili ili akusaidie ktk hili.
2.Endapo kama hakuna wosia au vikwazo vingine vyovyote vile vya kisheria, Makundi ya Warithi halali wa Mali za marehemu wanaotambulika kisheria ni hawa wafuatao:-
1) Mwenza au Wenza wa Marehemu.
2) Watoto wa Marehemu.
3)Wazazi wa Marehemu.
NOTE:- Kwenye makundi yote hapa juu, Sheria haijaainisha Jinsia ya Mrithi.
Aidha, watajwa hapa juu ni kundi la Kwanza kabisa la watu ambao Wana haki ya moja kwa moja ya kurithi mali za marehemu. Kuhusu makundi mengine ya warithi wengine endapo kama watajwa wote wa hapo juu hawapo, pata ushauri wa Wakili aliye karibu nawe.