Msaada, kuna kitu sielewi kwenye kalenda

Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
28,317
2,000
Wiki inasiku Saba
7×2=14
Mwezi una wiki nne
7×4=28

Mwezi wa pili huwa na siku 28

Sasa hii miezi yenye siku 30,32 hizi siku huwa zinatokea wapi
Warumi wa zamani kama ustaarabu wa zamani kabla yao, walitegemea dhana yao ya mwezi juu ya Mwezi. ... Julius Kaisari alibadilisha kalenda ya Kirumi mnamo 46 K.K kufanya kila mwezi uwe na siku 30/31, isipokuwa Februarius, ambayo ilikuwa na siku 28/29 na kupata mwaka wa nne wa ziada.
 

toughlendon_1

JF-Expert Member
Feb 7, 2018
2,733
2,000
Hii hesabu ingekuwa ndio mtihani wako wa kwenda peponi ungefeli ? Okay, kabla hujaijua kalenda unatakiwa ujue hesabu za kujumlisha, kuzindisha, kugawanya na kutoa..

KIURAHIS KABISA
Iko hivi: Wiki ina siku saba(7) hii ni costant, sawa ?

Mwezi una siku kuanzia 28-31 hii ni costant pia...

naomba usichanganye hivyo vitu viwili mzee KWAHIYO , Kwene mwezi wa siku 28 kuna wiki nne na kwa mwezi wa siku 31 kuna wiki nne pia na siku mbili tuki approximate 31/7=4.42 ~4 so inabid na yenyewe iwe nne.

MKUU NI LUNCH TIME KULA UGALI MKUBWA NA SAMAKI alafu comeback na mawazo mapya, tuendelee kuijenga hii nchi
 

GKado

JF-Expert Member
Oct 7, 2017
574
1,000
Hamna mwezi wenye siku 32...
Hahaha umenikumbusha ticha mmoja wa histori alienda kufundisha form one akasema ulizeni tarehe za matukio yote nitajibu na kuelezea kila tukio na tarehe husika, watoto waliuliza kila tarehe ticha anashuka nondo.
Dogo mmoja bright akampiga swali la mtego eti February 30 mwaka 1962 TANU walifanya tukio gani kubwa sana maeneo ya Lumumba, Ticha alishuka nondo huku wanafunzi wanacheka balaa.​
 

Jiwe_Tanzania

JF-Expert Member
Jun 26, 2018
412
1,000
Hahaha umenikumbusha ticha mmoja wa histori alienda kufundisha form one akasema ulizeni tarehe za matukio yote nitajibu na kuelezea kila tukio na tarehe husika, watoto waliuliza kila tarehe ticha anashuka nondo.
Dogo mmoja bright akampiga swali la mtego eti February 30 mwaka 1962 TANU walifanya tukio gani kubwa sana maeneo ya Lumumba, Ticha alishuka nondo huku wanafunzi wanacheka balaa.​
Na hapo bila shaka walianza kutilia wasi hata majibu yake ya mwanzo.
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
3,417
2,000
Mwezi mmoja ni muda (unaopimwa katika siku, kila mmoja ikiwa na wastani wa saa 24) wa gimba mwezi angani kukamilisha mwendo mmoja kuizunguka Sayari Dunia. Sasa, mwezi huu angani hukamilisha mzunguko wake mmoja kwa idadi ya siku tofauti, mathalani siku 28, 29, 30 ama 31 kutegemea na obiti ambayo mwezi hupitia kuizunguka dunia. Mwezi kuikamilisha mizunguko hiyo 12, tunapa mwaka mmoja. Na ndiyo wastani wa muda ambao dunia hukamilisha mwendo mmoja kulizunguka jua. Wiki moja (siku 7), ni wastani wa robo ya mwendo wa mwezi kuizunguka dunia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom