Msaada kuku wa nyama

Msaada kuku wa nyama

Chuck j

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2011
Posts
2,366
Reaction score
834
Naomba msaada kujua,,kuku wa nyama mia mbili wankula mifuko mingapi ya chakula?je na madawa garama zikoje?.pls kwa anaejua,,natanguliza shukrani
 
kwa vyakula vya kuku walivovichakachua ni ngumu kusema coz vikuku havikui hizo hesabu za kuku 100 kwa mifuko 4 ilikuwa miezi mitano nyuma lakini sasa hivi ni ngumu wanaweza wakala hata mifuko kumi na kuendelea
 
Naomba msaada kujua,,kuku wa nyama mia mbili wankula mifuko mingapi ya chakula?je na madawa garama zikoje?.pls kwa anaejua,,natanguliza shukrani

Hapa kila mtu atakuja na formula inayofanya kazi kwake, mfano mimi ni gunia 17za kilo 50 kwa muda wa wiki tano kuku mia tatu!
Kuku mmoja angalau anatumia kilo 2.5 mpaka anatoka, hivyo kuku 200, kwangu ni 2.5 * 200= 500/50(kilo ya mfuko mmoja)=10.
Hivyo kwa formula yangu ni mifuko 10.
Madawa kuna chanjo, vitamins na dawa za dharura kama mafua nk. Weka kando kama 80,000.
Ushauri zaidi subiri wataalam, hii ni yangu ambayo kwa kiasi imefanya kazi ila sio rasmi.
 
Barafu yamoto ,,,asante kwa udadavuaji wako unaosema si rasmi...kwangu ni mzuri sana na umenipa moyo sana,,,je chakula cha kampuni gani ni kizuri ?swali la pili kwanini hao wanaochakachua chakula cha kuku wanaachwa?
 
Back
Top Bottom