Msaada kujenga Ukumbi

Msaada kujenga Ukumbi

Bluetooth, Cejo, Mito, MahinaVeteran, Fall Army Worm, Hornet, Da Pretty, Coturnix, IPILIMO na Kifaru 1

Imekuwa ni Muda sana toka nilete mrejesho wa huu mradi. Na bila kupoteza muda napenda niwajulishe kuwa kama mshawahi kusikia Cash Cow ni huu mradi. Kwa sababu ya ukubwa wa eneo unaweza kufanya vitu vingi sana. Kwa sasa Kuna jamaa huwa wameukodi ukumbi Jumatatu hadi Alhamis kila jioni kuna watu wanatumia kama gym. Ijumaa hadi Jumapili Harusi.

Na Jumatatu hadi Ijumaa asubuhi ni nursery school. Mwenye nafasi ya kufanya huu mradi ningependa kumpa moyo FANYA. Kitu ambacho ningependa niwaambie tumia mtaalamu kwenye DESIGN YA JENGO. Mengine ya feasibility study, watu wa research kama mradi utalipa, marketing sijui nini achana nayo. Huyo mchoraji muombe tu akadirie material BASI. Ndugu zangu ukifuata mambo ya wataalamu watakupiga hela tu bila sababu. Nitawapeni mfano mwingine HAI KABISA.

Kuna mtu alinifuata kwenye in box. Akasema kaka nataka kujenga guest sehemu fulani akaitaja. Nikamwambia mpaka sasa umefanya nini? Akaniambia ameenda kwa injinia kamwambia aende kwa watu wa research wamtizamie kama soko lipo, kwa mchoraji, kisha aende kwa mtu amtengenezee gharama za material ya ujenzi.
Nilimwambia tengeneza mchoro na pitisha manispaa, kingine si lazima injinia mtu anayeweza kujenga tu mwenye profile ya kawaida atakujengea fanya finishing nzuri basi. Baada ya muda alikuja kunishukuru kuwa haikuwepo haja ya research. SI KILA KITU KINA HITAJI RESEARCH fikiri kwanza wateja huwa hawatoki karibu na guest.

Nawashukuru sana kwa interest zenu wadau mwisho kabisa MRADI WA SHULE HAUMTUPI MTU. Fikiria mtoto mmoja wa nursery 40,000 na wa msingi ni 80,000 kwa mwezi hizi za uswahilini kwa mwaka nihela nzuri ukiwa nao 100? 200? 300? kumbuka walimu wana mishahara ya kawaida tu. Kingine kitu kikubwa cha kukumbuka hii miradi haikai Samora avenue wala Masaki hukoo nje ya mji bei ya ardhi unaweza imudu. Usione shida kufungua shule ya darasa moja huko Kibaha, Gezaulole na sehemu kama hizo.

Mungu awabariki sana na ninashukuru sana sana kwa interest zenu na challenge mlizonipa.
Imeniinspire kusema kweli. Ila natamani kusikia kidogo kuhusu location, vip haimati kwa biashara ya Ukumbi?
 
Back
Top Bottom