Msaada Kuhusu zoezi la uhakiki taarifa za Mpiga kura

makofia360

JF-Expert Member
May 28, 2015
776
2,379
Naona ndoto ya kupiga kura katika familia yetu ya watu saba imetanda giza. Hiyo ni baada ya kuangalia kapitia mobile system kwa namba waliyotuelekeza lakini system imeshindwa kutambua namba zetu ikatuelekeza twende ofisi za kata, Hatukusita tukaenda kibaya zaidi taarifa zetu wote hazikuwepo na kwa nilivyoona inawezekana ni watu wengi hawapo. Swali je Kama taarifa zako hazipo hutaweza kupiga kura?





====================
====================



 
Mkuu hii ni shida kubwa naona goli la mkono limeanza. Hapa Iringa watu wengi wamekuta majina yao hayamo kabisa pamoja na kwamba wana vitambulisho. Viongozi wa vyama inabidi waingilie kati vinginevyo..
 
Huku yani ni shida katika kata na majina niliyoyaona hayazidi 40 na watu walijiandikisha wengi kweli,,,natafakari kwa mfumo wa bvr ilikuwa na ulazima wa kuhakiki kweli? lisipo angaliwa hili tatizo hatutapiga kura wengi
 
Sijajua ila ukikuta jina halipo c unampa kitambulisho akujumuishe kwenye daftari la mpiga kura
 
Aisee nilifikiri mi peke yangu!
Mi nimemfuata diwani nikamweleza,akasema haina shida kura nitapiga tu,cha muhimu ni kwenda kuangalia jina km lipo kwny daftar yatakayobandikwa ulipojiandikishia
 
Huku kwetu Iringa jamaa wa NEC wamekuja kimya kimya na wananchi hatukupewa taarifa. Kwenda leo tunasikia wameondoka jana. Kuangalia majina mengi hayamo ingawa vitambulisho tunavyo, huko kwingine kaa chonjo
 
Hilo limetokea pia mtaani kwangu ambapo watu 1080 waliandikishwa lkn ni majina 269 tu ndio yaliyoonekana kwenye daftal. Hili ni tatizo tena kubwa
 
Ok ndugu viongozi bila shaka mmelisikia hilo tatizo, tunataka majibu otherwise siku ya uchaguzi patachimbika...mimi najua hili zoezi la uhakiki linaloendekea ni kucheck makosa labda kwenye herufi za jina, au jinsia au tarehe ya kuzaliwa e.t.c Ila sitegemei eti jina la mtu lisiwepo wakati ana kitambulisho kinachoonesha Kata na kituo alichojiandikishia..
 
Nimejiandikisha na kitambulisho pia kipo.Na ni Mtanzania halali
 
Nasikia eti walioenda kuhakiki ndo siku ya kupiga kura wataambiwa wameshapiga. Kuwa makini
 
makofia360 naomba uirudie ile namba ya NEC tena maana nimeisahau
kwani hata mm nilishaitumia mara ya kwanza na majibu ya Tume ni kuwa namba yangi haipo niende kwenye kituo cha Kata kuhakiki tena
 
hivi hamkwenda kucheki taarifa zenu kwenye ofisi za kata 7-11 august kwa mikoa yote? kama jina liko humo ndo kwa muhimu haya mambo ya mitandao kwa setting zetu sidhani kama yako active sana.

kama mpo Dar au zanzibar nenda kwenye ofisi ya kata bado deadline haijapita.
 
Kwakweli hili ni tatizo na Lisipo angaliwa kwa Makini itaku shida wakati wa upigaji wa kura
 
Nami imegoma aisee sijui kuna kamchezo gani kanaendelea halafu kwa viongozi wa CDM taifa wilaya MVOMERO MOROGORO watu wameongezwa kiujanja na kufikia 18000 wakat maafisa wamehakiki watu wapo wachache tofaut na hyo idadi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…