Msaada kuhusu VISA ya UK visit..

Msaada kuhusu VISA ya UK visit..

New Nytemare

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2011
Posts
3,400
Reaction score
2,572
Nimeomba UK visit visa miezi 6 nimekosa kwasababu mbali mbali moja wapo ni kuwa hawana uhakika kama nitarudi tena bongo pia hakuna genuine relationship Kati ya mimi na sponsor, nataka kuomba tena naomba ushauri wenu wana JF kwa watu wenye experience ya UK visit visa.
maana nina rafiki yangu huko kaniarika niende..sasa sielewi nifanyaje ili nipate kiurahisi..
 
msaada wadau
Lbda nikuambie ni wengi wanaonyimwa visa za UK. Nadahni hata uki-apply tena kiharaka haraka utakosa tena. Hilo swala la ''hawana uhakika kama utarudi Bongo'' ndio issue kubwa. Hili unaweza kulionyesha kwa kuwa na kazi nzuri /biashara, ya uhakika na yenye kipato kizuri hapa Bongo, hivyo wanakuwa na uhakika kuwa huwezi kuviacha na ukazamia. Kuna issue nyingine kama kuwa na familia au mali kama nyumba nk. Najua jamaa wengi walio-apply kwa kigezo cha kwenda kutembea au graduation ya fulani na wakafeli
 
nitumie ujanja gani kiongoz
huyu ninaenda kumtembelea ni mpenzi wangu
 
Una shughuli gani inayokuweka mjini?
Umri wa wazazi wako pia husaidia ukisema wanakutegemea wewe kuwapeleka hospital wakiugua hivyo huwezi kukaa sana. Ikiwezekana omba mitatu tu mingine unaongeza ukishaingia
 
Nimeomba UK visit visa miezi 6 nimekosa kwasababu mbali mbali moja wapo ni kuwa hawana uhakika kama nitarudi tena bongo pia hakuna genuine relationship Kati ya mimi na sponsor, nataka kuomba tena naomba ushauri wenu wana JF kwa watu wenye experience ya UK visit visa.
maana nina rafiki yangu huko kaniarika niende..sasa sielewi nifanyaje ili nipate kiurahisi..

Wakati mwingine hata mood ya Consular inaweza kuchangia kupata au kukosa.

Ingawa 'Strong Social Ties (Family,Employment,Financial)'
Zako wewe muombaji hapa nyumbani zinaangaliwa.

Lakini, Lakini, - Huyo mwenyejiwako wako nae huko aliko status yake na anachokifanya kimaisha chaweza kuwa na mchango pia.

Kuhusu kuomba tena,
Jitafakari mwenyewe maana inategemewa kama unarudi tena ndani ya muda mfupi bila shaka unapeleka viambatanisho vingine tena zaidi pengine na sababu zenye mashiko zaidi.
Sio sababu ileile, barua zilezile na kwa kawaida yetu Wabongo hata kujibu maswali tumesha-crame zis,zea,endzen zilezile,
Huwa hawapotezagi muda,
Utasikia- Neeeeext!
 
Back
Top Bottom