Msaada kuhusu uwiano wa chakula cha kuku

GANG MO

JF-Expert Member
Dec 6, 2016
2,087
2,193
habari ya majukumu ya kutwa wadau wa kilimo na ufugaji. samahani nimeanza ufugaji wa kuku wa kienyeji. nina kuku 30 wa miezi 5 na 6. naombeni kujuzwa kuhusu namna ya kuwapimia chakula. je kuku 30 wanakula kiasi gani? nawasilisha
 
hello wadau
 
Kila kuku mmoja anahitaji walau gramu 0.125 za chakula Kwa siku hivyo basi Kwa hao kuku 30 andaa walau kilo 3.75 za chakula
 
Lakini njia nzuri zaidi uwe unafatilia tu ulaji wao wa chakula,kadiria chakula, kuku wakila vizuri wakashiba utaona tu wametulia na hawasumbui
 
Hivi unajua kuku wewe au ndio tunachangia tu kila kinachokuja mbele yetu? Yaani kuku uwape chakula mpaka utakapoona wametulia?

Let's get serious huyu mtu kauliza swali anahitaji msaada
 
habari ya majukumu ya kutwa wadau wa kilimo na ufugaji. samahani nimeanza ufugaji wa kuku wa kienyeji. nina kuku 30 wa miezi 5 na 6. naombeni kujuzwa kuhusu namna ya kuwapimia chakula. je kuku 30 wanakula kiasi gani? nawasilisha
Kuku wa umri huo wanakula grams 130 kwa siku, hiyo ni sawa na kilo 1.3 kwa kuku kumi. Kwa hivyo kuku wako 30 wanahitaji kilo jumla ya kilo 4 ya chakula kwa siku ambayo unawapa kilo 2 asubuhi na kilo 2 jioni

Zingatia mchanganuo huu ni kama Unatumia chakula chenye mchanganyiko sahihi kwa ajili ya kula kuku. Kama unatumia pumba plain utahitaji kuwapa zaidi ya kiasi hicho

Ukihitaji kujua namna ya kuchanganya chakula cha kuku Sema nitakupa formula
 
hello wadau
Hongera kwa kuanzisha mradi wa ufugaji kuku wa kienyeji.
Zingatia yafuatayo ili mradi wako uwe ni endelevu na wenye Tija.
1. Kuku mmoja anahitaji grams 120 za chakula kwa siku. Kwa mantiki hiyo kama unawalisha mara mbili kwa siku itakubidi ulishe grams 60 kwa kuku mmoja asubuhi na urudie grams 60 kwa kuku mmoja jioni ili kukamilisha grams 120 kwa siku kwa kuku mmoja. Kwa hiyo kuku 30 utawalisha grams 120 kwa kuku mmoja x idadi ya kuku 30 = grams 3,600(sawa na kg 3.6). Kwa kawaida gunia moja la chakula cha kuku lenye uzito wa Kg.100 litatosha kuwalisha kuku wako 30 kwa siku 28 - roughly ni mwezi mmoja. Kwa hiyo kila mwezi ujue utatakiwa uwe na gunia la chakula cha kuku wako.
2. Chakula cha kuku kinatakiwa kiwe ni mlo kamili (Balanced diet). Yaani kiwe na protini,wanga,madini vitamins na bila kusahau maji ya kunywa yakutosha. Usiwaache wazurure kujitafutia chakula (Kubangaiza) wao wenyewe la sivyo ugonjwa wa kideri, ndui na kuharisha(kindupindu i.e.Fowl cholera) vitakusumbua sana. Katika banda lako hakikisha kuku hawasongamani na hakuna unyevunyevu ili kuepuka mlipuko wa ugonjwa wa mafua ya kuku/ndege.
3.Unaweza kuchanganya au kutengeneza (Formulate) chakula cha kuku wewe mwenyewe kwa kutumia mali ghafi zinazopatikana kwenye mazingira yako kwa gharama nafuu badala ya kutegemea kile cha madukani ambacho huna uhakika wa ubora wake sana.(Maelezo yanayoandikwa nje ya mfuko wa chakula cha madukani yapo kibiashara zaidi.
4. Uwe unapata ushauri wa kitaalam mara kwa mara.
 
Kila kuku mmoja anahitaji walau gramu 0.125 za chakula Kwa siku hivyo basi Kwa hao kuku 30 andaa walau kilo 3.75 za chakula
Kama lengo ni kumuua huyo kuku kwa njaa basi utampa hizo gramu 0.125 za chakula kwa siku. Lakini kipimo sahihi kwa kuku mmoja wa umri huo ni kati ya gramu 120 na 130 kwa siku.
 
Kuku wa umri huo wanakula grams 130 kwa siku, hiyo ni sawa na kilo 1.3 kwa kuku kumi. Kwa hivyo kuku wako 30 wanahitaji kilo jumla ya kilo 4 ya chakula kwa siku ambayo unawapa kilo 2 asubuhi na kilo 2 jioni

Zingatia mchanganuo huu ni kama Unatumia chakula chenye mchanganyiko sahihi kwa ajili ya kula kuku. Kama unatumia pumba plain utahitaji kuwapa zaidi ya kiasi hicho

Ukihitaji kujua namna ya kuchanganya chakula cha kuku Sema nitakupa formula
Ahsante sana kwa wako ushauri. Mungu akubariki. Naomba unisaidie hiyo formula

Sent using samsung galaxy grand prime pro
 
Hongera kwa kuanzisha mradi wa ufugaji kuku wa kienyeji.
Zingatia yafuatayo ili mradi wako uwe ni endelevu na wenye Tija.
1. Kuku mmoja anahitaji grams 120 za chakula kwa siku. Kwa mantiki hiyo kama unawalisha mara mbili kwa siku itakubidi ulishe grams 60 kwa kuku mmoja asubuhi na urudie grams 60 kwa kuku mmoja jioni ili kukamilisha grams 120 kwa siku kwa kuku mmoja. Kwa hiyo kuku 30 utawalisha grams 120 kwa kuku mmoja x idadi ya kuku 30 = grams 3,600(sawa na kg 3.6). Kwa kawaida gunia moja la chakula cha kuku lenye uzito wa Kg.100 litatosha kuwalisha kuku wako 30 kwa siku 28 - roughly ni mwezi mmoja. Kwa hiyo kila mwezi ujue utatakiwa uwe na gunia la chakula cha kuku wako.
2. Chakula cha kuku kinatakiwa kiwe ni mlo kamili (Balanced diet). Yaani kiwe na protini,wanga,madini vitamins na bila kusahau maji ya kunywa yakutosha. Usiwaache wazurure kujitafutia chakula (Kubangaiza) wao wenyewe la sivyo ugonjwa wa kideri, ndui na kuharisha(kindupindu i.e.Fowl cholera) vitakusumbua sana. Katika banda lako hakikisha kuku hawasongamani na hakuna unyevunyevu ili kuepuka mlipuko wa ugonjwa wa mafua ya kuku/ndege.
3.Unaweza kuchanganya au kutengeneza (Formulate) chakula cha kuku wewe mwenyewe kwa kutumia mali ghafi zinazopatikana kwenye mazingira yako kwa gharama nafuu badala ya kutegemea kile cha madukani ambacho huna uhakika wa ubora wake sana.(Maelezo yanayoandikwa nje ya mfuko wa chakula cha madukani yapo kibiashara zaidi.
4. Uwe unapata ushauri wa kitaalam mara kwa mara.
Ahsante sana kwa wako ushauri mzuri. Mungu akubariki

Mkuu uwa unatengeneza chakula cha kuku wako na unapata matokeo mazuri kama au zaidi ya ambavyo ungenunua chakula cha dukani? Kama ndivyo naomba hiyo formula yako unayotumia kwenye kuchanganya hicho chakula.
 
Ahsante sana kwa wako ushauri mzuri. Mungu akubariki

Sent using samsung galaxy grand prime pro
emoji120.png
emoji120.png
 
Kuku wa umri huo wanakula grams 130 kwa siku, hiyo ni sawa na kilo 1.3 kwa kuku kumi. Kwa hivyo kuku wako 30 wanahitaji kilo jumla ya kilo 4 ya chakula kwa siku ambayo unawapa kilo 2 asubuhi na kilo 2 jioni

Zingatia mchanganuo huu ni kama Unatumia chakula chenye mchanganyiko sahihi kwa ajili ya kula kuku. Kama unatumia pumba plain utahitaji kuwapa zaidi ya kiasi hicho

Ukihitaji kujua namna ya kuchanganya chakula cha kuku Sema nitakupa formula
Habari. samahani plz naomba formular ya mchanganyiko wa chakula cha kuku 0753008888
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom