Msaada Kuhusu ufugaji wa kuku wa mayai

Brown Mduma

Senior Member
Sep 29, 2020
180
283
Wakuu mwenye kujua changamoto za ufugaji wa kuku wa Mayai na namna kuzikwepa anipe muongozo kidogo kwasababu kuna jamaa mmoja alinisimulia juu juu tu kuhusu ufugaji huo akidai nikiwa na kuku 300 niweza pata hadi trey 18 kwa siku kuku wa kishaanza kutaga sasa kwa upande wangu nimeona ni fursa nzur kama naweza nikakomaa nayo vizuri inaweza kunitoa kimaisha maana mtaani pagumu sana wakuu.

Nia Yangu ni kwamba ni pangishe chumba kikubwa ambacho hata kisipokuwa na umeme sawa lkn niwe nawafuga kwenye chumba cha 10×10 at least au kinachozidi hicho ambacho kipo uswazi kodi isiyozidi 30 kwa mwez. Na vile ningependa kujua ninaponunua vifaranga(mbegu) vitachukua mda gani kufika kuanza kutaga.

Ambae anaexperience na ufagaji huu naomba usisite kunipa muongozo mzur ili niweze kuanza niwe nishajua nini chakufanya.
 
Pata nafasi watembelee wafugaji wanaofuga physically ujue uhalisia ugumu na uzuri wake maana biashara za kusikia zitakutoa kwenye reli
 
Back
Top Bottom