Msaada kuhusu ubora wa tairi za good ride

BRO SANTANA

JF-Expert Member
Jun 15, 2015
1,845
2,247
Jamani nafikiri ni wazima.

Naomba kujua ubora wa tairi hizi za Good ride toka china maana kuna mtu anataka kuniuzia used lakini zina hali nzuri.
 
Kama ni used, angalia kama muda wa matumizi haujafika kikomo. Muda wa kuzalishwa tairi kiwandani unaandikwa ubavuni mwa tairi husika, katika mfumo wa wwyy yaani wiki na mwaka. Kwa mfano 4112 inamaanisha tairi ilizalishwa wiki ya 41 ya mwaka 2012, na ubora wake hudumu kwa miaka 4. Baada ya hapo kutumia tairi iliyoisha muda wake, NI HATARI.
 
Nashukuru mkuu lkn naomba kujua ubora wake zaidi hasa kwa rafu road na safari ndefu.
 
Mimi mwenyewe nayatumia, sijawahi hata kupata burst, yakichoka natafuta mengine. Ila kama uwezo upo, nunua mapya kwani waweza tumia hata miaka 4 (kutegemeana na barabara unazopita)
 
Mkuu kwa tyre za uchinani ling long ni nzuri au champiro hayo mengine ni ubaishaji waweza tembea km400 unashangaa zinavimba nyingine unaganyaga kajiwe kenye ncha dhaifu inachanika.
 
Nimeexperince hili kwa wengi c mbaya ukawaona hata wabadilishaji watyre watakwambia kwa uzoefu wao
 
Funga bridgestone continental au kama una pesa funga pirelli kwisha habar.
 
Tyre za china then used?hapana,bora ukanunue mpya. Tyre za china mara nyingi zinakaa mda mfupi
 
nina uzi wangu wa matairi ya bridgestone. unaweza kucheki huo uzi.
ila naona kwa wewe bajeti yako umeshazoea kununua matairi used.
siku ukitaka matairi super brand na quality yanayodumu muda mrefu nitafute.
 
Nyoosha mkono kidogo,nunua Moya moja itakuwa kuanzia 130k kulingana na ukubwa Wa rim
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom