Habari waungwana!
Naomba kuuliza "hivi usajili wa hii bahati nasibu ya waliochoka kuishi nchini kwao kama mimi unaendeshwa na kampuni binafsi?
Maana naona kila nikisajili mwishoni kaharufu cha utapeli kanakuja, wananiomba ada ya usajili. Mimi mgumu sana kutapeliwa mtandaoni.
Aliyewahi kushinda bahati nasibu hii au anayejua vizuri naomba aniambie je, kuna ada yoyote ya usajili au nimeingia tovuti feki?