Nawakumbusha Wacheza Kamari kwamba, Kamari ni haram ila USA Green Card Lottery Tayari imeshafunguliwa

PakiJinja

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
7,652
15,770
Najua kuna wacheza kamari tayari wameshacheza, wengine hawana taarifa na wengine wamesahau. Naomba nitumie uzi huu kuwakumbusha wale wote walio tayari kucheza USA Green Card Lottery, kwamba, dirisha limeshafunguliwa na wacheza kamari kutoka nchi mbalumbali wanacheza kwa bidii kujaribu bahati zao. Ikumbukwe, kucheza kamari ni haram kama ilivyo haram kula nyama zilizo katazwa, ingawa kuna nchi ni kama hazizingatii kabisa hili na unaweza ukaona namna raia wa nchi hizi walivyoongoza katika mchezo huo wa kamarim.

Nchi zilizoongoza kwenye USA Green Card Lottery program.
▪ Egypt — 5,529

▪ Algeria — 5,526

▪ Iran — 5,506

▪ Russia — 5,505

▪ Sudan — 4,863

▪ Morocco — 4,469

Hii ni fursa na natoa wito watanzania kuchangamkia fursa hii. Angalia safari hii, Tupate watanzania zaidi ya 165 wa safari iliyopita na mfike angalau 1000+.
Niwatakieni kila la heri.
Zingatieni sana maelekezo: Electronic Diversity Visa Program
 
Hahaha nyumbani kumenoga jamani, DP world wakipewa bandari kila mtu atapata zaidi ya bilioni moja, nyie mnataka kuzikimbia hizo.
 
Mkuu naomba unisaidie niweze kui apply hii kitu nimeshatafuta sana namna ya kuomba nashindwa
Mkuu, just fuata maelezo yaliyotolewa humo, yapo very straight. Yakikutatiza uje na swali specific. Humu kuna wajuzi, haitashindikana.
Kuhusu kuomba na kutopata, kumbuka hii ni Kamari tu, hivyo bahati haijawa upande wako ingawa kuna namna unaweza ukajiongezea chances za kushinda. Mfano, kama una ndoa basi himizaneni, wote wawili wewe na mwenza wako mjaze kila mmoja kivyake huko like marriage status mnajumuishana. Hapo mnakua mmejiongezea chances za kushinda, sababu huenda mmoja kati yenu akabahatika. Pili kama mna watoto hiyo pia inaongeza chance kwani wanahitaji watoto wakawalee katika mfumo wao.
So, kuna vi factors ambavyo siyo vigezo bali vina add value tu.
 
Nadhani kabla ya mtu kutuma maombi apitie kupata elimu kwenye passport size wanayo hitaji laa sivyo itakua ni kupoteza muda tu.
Kwa Sababu wengi wanaokosa ni kutokana na passport size isio kidhii vigezo.
 
Back
Top Bottom