Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,633
- 697,754
American green card lottery... Ni mpango mkakati wezeshi uliobuniwa na wamerakani kutoa nafasi kwa njia ya bahati nasibu kwa washindi wa nchi maskini kuingia kuishi na kufanya kazi Marekani kunakotajwa kuwa na nafuu ya maisha
Mpango huu tangu uanzishwe umefaidisha nchi nyingi za dunia ya tatu kwa raia wake kwa maelfu kupata nafsi hiyo adhimu... Lottery hii hufanyika kila mwaka na huwa kuna nafasi elfu 50 za kushindaniwa..
Tanzania ni mmojawapo wa mataifa wafaidikaji wa huu mpango.. Wapo Watanzania wengi tu leo hii wanaishi marekani kupitia mpango huu.
Wiki hii kwa mstuko mkubwa kabisa pamoja na mambo mengine yaliyoipata nchi yetu kimataifa ni pamoja na hili la ZUIO la Watanzania kushiriki bahati nasibu tajwa... Kwa maana ya kwamba kwa mwaka huu hakuna mtanzania atakayeruhusiwa kushiriki
Mambo yaliyotokea wiki hii kwa mfululizo wa pamoja yamewachanganya wengi na kujikuta nao wamechanganya mambo pia..
Zuio la kushiriki bahati nasibu ya kadi ya kijani halina mahusiano ya moja kwa moja na zuio kikwazo cha baadhi ya viongozi kuingia Marekani...
Yani kuna orodha ya viongozi wa serikali ya Tanzania wamewekewa ZUIO la kuingia Marekani kutokana na tuhuma kadha wa kadha... ZUIO hili halina mahusiano na zuio la kushiriki bahati nasibu.. Yaani Watanzania wote ambao hhawatawekwa kwenye ZUIO la kuingia Marekani wataruhusiwa kuingia Marekani kwa malengo na shughuli mbalimbali
Kisichojulikana na wengi ni kwamba ZUIO la viongozi wa serikali ya Tanzania kuingia Marekani ni la ndani ya nchi na linawahusu baadhi ya viongozi wa serikali ya Tanzania wenye tuhuma zilizoainishwa... Wakati ZUIO la kushiriki bahati nasibu ya kuishi na kufanya kazi Marekani ni la kikanda na kimataifa
Kwenye haya mazuio mawili kila upande husika una mzigo wa lawama... Zuio la viongozi litaambatana na vikwazo vingine, kunyimwa ama kupunguziwa misaada.. Kupelekwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu nknk.. Nchi inatiwa DOA na kulaumiwa ni viongozi
Zuio la kushiriki bahati nasibu ya kuishi na kufanya kazi Marekani hili linawahusu Watanzania katika ujumla wao... Na hapa kama taifa lawana hii ni yetu sote... Watanzania tumekuwa watu wa hovyo... Rahisi kununulika na kuwa manipulated kwa njia nyingi tu
Pesa kidogo inaweza kumnunua mtanzania na kumtumia kutimiza malengo yako... Maelfu ya vijana wetu wako kwenye magereza mbalimbali duniani kwa ishu za uhalifu lakini unapofuatilia kwa karibu unakuta hawana wajuacho zaidi ya kugundua kuwa walitumika na watu ambao hata hawawajui vema...
UGAIDI jambo hili la kutisha... Umekuwa ni vita ngumu sana duniani na sheria ngumu nyingi zimetungwa ili kuweza kuukabili... Tanzania iliyojulikana kwa ustaarabu, ukweli na uaminifu hapo mwanzo sasa ni mojawapo ya mataifa yanayosemwa vibaya... Na kwa bahati mbaya sana hatimaye imetajwa raia wake kushiriki ugaidi mbalimbali duniani
Ukiangalia mataifa yaliyowekewa ZUIO la kushiriki bahati nasibu ya kadi ya kijani.. Ni mataifa yenye DOA kubwa la mambo ya kigaidi... Tanzania imekuwaje mpaka kujumuishwa hapa?
Kama taifa kuna mahali tulijisahau na tukaruhusu wageni wakatuingilia kwa pesa kidogo tu huku tukiruhusu vijana wetu kushirikiana na wageni tusiowajua vema huku tukiwaruhusu wasafiri ughaibuni bila kujua kwa hakika huko waendako wanaenda kufanya nini...
Matokeo yake vijana wetu wakaishia kuingizwa kwenye makundi ya kigaidi na kufundishwa ugaidi... Mwisho wa yote ninini? Matukio ya kigaidi yalipofanyika na baadhi ya washukiwa kukamatwa Watanzania hawakukosekana! Taswira ya Taifa inachafuliwa...
Ukarimu wetu uliopitiliza na kupenda pesa bila kujali uzalendo na matokeo ya matendo yetu haya kumesababisha kuruhusu wageni maharamia kumiliki nyaraka zetu muhimu kama vitambulisho vya Taifa na hati za kusafiria... Kwahiyo sometimes wanaokamatwa sio Watanzania lakini wana nyaraka za Tanzania... Unajiuliza WAMEZIPATAJE?
Kwahiyo tusichanganye madesa ishu ya ZUIO la kushiriki bahati nasibu ya kadi ya kijani halina mahusiano kabisa na serikali bali ni letu wenyewe kwa ujuha na upumbavu wetu
Jr