Msaada kuhusu tatizo la sonona

Msaada kuhusu tatizo la sonona

Poluyakhtov

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2017
Posts
365
Reaction score
306
Habari za asubuhi wana JF,
Kama kichwa cha thread kinavyojieleza, kuna ndugu yangu wa kiume mwenye umri wa miaka 30. Yeye ni mhitimu wa chuo kikuu miaka 5 iliyopita, alisomea Bachelor of Human Resources Management.
Alipohitimu tu;akabahatika kufanya kazi ya muda kwenye ofisi moja ya shirika la umma. Kazi hiyo hakudumu nayo sana kwani aliarifiwa kuwa kazi hiyo ilikuwa imemalizika.
Tangu hapo, mdogo wangu amekuwa ni mtu wa huzuni na kukata tamaa, na kuna muda anawaza hata kujitoa uhai, hasira hata kwa vitu vidogo tu. Hata kulala kwake ni mtihani. Anamuona kila mtu kama adui kwake.
Natamani sana kumsaidia ndugu yangu, tatizo sijui nianzie wapi au ni hospitali ipi inatoa huduma kwa matatizo kama hayo.
Naomba msaada wa maelekezo wa sehemu husika na gharama kama itawezekana.
Asanteni.
 
Hayo matatizo yake yanawezekana kupona Ila ni vizuri ukampa Biashara endapo hajapata ajira.
Mfundishe namna sahihi ya Ku-lower expectation .

Mediation n.k

Ikiwa hana Kazi hana Biashara ni rahisi Sana kuwa depressed , heart fainted hasa kwa kijana mwenye age hiyo
 
Asante Aaliyyah kuniita,
Hii ni changamoto kwa graduates wengi Tanzania. Watu wamemaliza vyuo miaka kumi hawana cha kufanya, akili zimekwama na hakuna mitaji wala maarifa ya kufanya biashara. Ni changamoto sana.

Mtu wa namna hiyo anahitaji ushauri, apunguze matarajio yake(huenda aliwaza kuajiriwa na makampuni makubwa, kupata mshahara mkubwa, kuishi maisha mazuri chini ya ajira nzuri). Aongozwe kujua kwamba alichofikiri na uhalisia ni tofauti, aongozwe kujitafuta kuanzia chini, afundishwe kujisimamia kibiashara. Ni ngumu sana ila inabidi iwe hivyo.

AJIRA HAKUNA, huo ndio ukweli. Na hali itazidi kuwa mbaya miaka 5-10 ijayo.
 
Amtafute bwana sungura azungumze naye vizuri
1000028893.png
 
Mtoa mada pitia hapa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom