Msaada kuhusu mafao ya NSSF..

Msaada kuhusu mafao ya NSSF..

mc1886

Member
Joined
Feb 6, 2013
Posts
33
Reaction score
0
Habari zenu wana jamii?
Naombeni mnisaidie mawazo, nina jamaa yangu mmoja alikuwa akifanya kazi katika kampuni flani hapa mjini (DSM) zaidi ya miaka 10. Ila ameacha kazi na hakuwa kwenye good terms na mwajiri wake wakati anaacha kazi hakupewa barua ya kuachishwa kazi. Anahitaji kufatilia mafao yake ya nssf. Je ni taratibu (procedures) gani anatakiwa azifuate ili alipwe mafao yake? na afanye nini endapo aliyekuwa mwajiri wake atagoma kumsainia papers zinazomthibitisha kuwa alikuwa mwajiriwa katika hiyo kampuni.? Mawazo yenu ni muhimu hapa.
 
Ajaribu kumuona mwajiri tena, maana barua ya kuacha kazi ni haki yake na Certificate of Service kisheria. Akikataa, basi aende CMA (Commission of Mediation and Arbitration) na mwajiri ataitwa huko huko. Afike pia ofisi za NSSF na kadi yake na watamjazia michango yake yote.

Labda kwa kuuliza tu aliacha kazi bila kufuata taratibu au?
 
Taratibu zimebadilika siyo kama zamani, aende NSSF alikokuwa anapeleka michango yake akiwa na kadi kisha awaeleze kuwa haendelei na kazi tangu tarehe so and so kisha atoe taarifa kwamba anataka kuchukua mafao yake. Itamchukua miezi 6 kupata sasa hivi hakuna kujaza mifomu kama zamani. Ikishindikana wakitaka barua ya muajiri basi aonane na HR manager wake ampe termination letter ili aweze kupata mafao yake.
 
mmh basi huku kwetu hatujahamia dijitali!, me nilifatilia last week nikapewa fomu na lazima muajiri wako asaini na barua ya kuacha kazi lazima uwe nayo.
 
na je kuna,njia yeyote ya kujua jumla ya nafao yako bila kwenda ofsin kwao yaani nssf?
 
Asante kwa ushauri wako, ni kweli aliacha kazi bila kufuata taratibu.
 
Ajaribu kumuona mwajiri tena, maana barua ya kuacha kazi ni haki yake na Certificate of Service kisheria. Akikataa, basi aende CMA (Commission of Mediation and Arbitration) na mwajiri ataitwa huko huko. Afike pia ofisi za NSSF na kadi yake na watamjazia michango yake yote.

Labda kwa kuuliza tu aliacha kazi bila kufuata taratibu au?
Asante kwa ushauri wako, yah! aliaicha kazi bila kufuata taratibu.
 
Taratibu zimebadilika siyo kama zamani, aende NSSF alikokuwa anapeleka michango yake akiwa na kadi kisha awaeleze kuwa haendelei na kazi tangu tarehe so and so kisha atoe taarifa kwamba anataka kuchukua mafao yake. Itamchukua miezi 6 kupata sasa hivi hakuna kujaza mifomu kama zamani. Ikishindikana wakitaka barua ya muajiri basi aonane na HR manager wake ampe termination letter ili aweze kupata mafao yake.

Asante sana mkuu kwa ushauri wako, nitamshauri afanye hivyo.
 
na je kuna,njia yeyote ya kujua jumla ya nafao yako bila kwenda ofsin kwao yaani nssf?

... Ndiyo kuna kitu inaitwa "NSSF MOBILE".
Unachotakiwa kuwa na namba yako ya uanachama wa NSSF nakuwa kwenye mtandao. Hapo kwa hapo unatumiwa kiasi ulichonacho kwenye Akaunti yako.
 
... Ndiyo kuna kitu inaitwa "NSSF MOBILE".
Unachotakiwa kuwa na namba yako ya uanachama wa NSSF nakuma kwenye mtandao. Hapo kwa hapo unatumiwa kiasi ulichonacho kwenye Akaunti yako.

hiyo process inakuwaje mkuu..hiyo number unaifanyaje kaka...
 
Asante kwa ushauri wako, ni kweli aliacha kazi bila kufuata taratibu.

Hapana kuhusu mafao yoyote Yale (Nssf, Ppf GEPF, pspf, etc) haijalishi uliacha kazi kwa kufuata utaratibu AMA la, lazima ulipwe haki zako na mwajiri hana mamlaka juu ya hilo
 
hiyo process inakuwaje mkuu..hiyo number unaifanyaje kaka...

... Sawa mkuu' nitakuwekea muda si mrefu. Ngoja nimalize jukumu' niko kwenye uzinduzi wa vitambulisha vya taifa, hapa kwenye viwanja vya Karimjee.
 
yeah...hata mimi nataka kujua mkuu

kuwa nasubira' naona kuna wengi wanaPM.
tafadhari nitaweka hapa muda si mrefu jinsi ya kupata hiyo kitu. "sorry for delay"
 
Habari zenu wana jamii?
Naombeni mnisaidie mawazo, nina jamaa yangu mmoja alikuwa akifanya kazi katika kampuni flani hapa mjini (DSM) zaidi ya miaka 10. Ila ameacha kazi na hakuwa kwenye good terms na mwajiri wake wakati anaacha kazi hakupewa barua ya kuachishwa kazi. Anahitaji kufatilia mafao yake ya nssf. Je ni taratibu (procedures) gani anatakiwa azifuate ili alipwe mafao yake? na afanye nini endapo aliyekuwa mwajiri wake atagoma kumsainia papers zinazomthibitisha kuwa alikuwa mwajiriwa katika hiyo kampuni.? Mawazo yenu ni muhimu hapa.

1. Kama ni NSSF, lazima apeleke form za michango iliyokuwa inapelekwa NSSF kutoka kwa mwajiri, fomu hizo inabidi huyo rafiki yako akachukue NSSF na kupeleka kwa mwajiri wake wa zamani. Hii inawasaidia NSSF kuhakiki michango iliyopelekwa na malipo waliyopokea wao.

2. Lazima awe na kadi ya electronic ya NSSF.
3. Apeleke barua ya kuacha kazi/kuachishwa kazi.

Mwajiri wa zamani anahusika sana kwenye kufuatilia mafao japo NSSF haiwahusu sana umeachaje kazi cha msingi kwao uwapelekee form za michango yao zilizosainiwa na mwajiri wako na barua ya kuacha/kuachishwa kazi.
 
hao jamaa wanasumbua sana,

coz kuna watu wengi wanajitoa kwenye huo mfuko.
 
hiyo process inakuwaje mkuu..hiyo number unaifanyaje kaka...

KUJUA KIASI ULICHO CHANGIA KWA WANACHA WA NSSF:
Fuata maelezo yafuatayo;

KWENYE SIMU YAKO TUMA UJUMBE MTUPU KWENDA 15747

utapata majibu yasemayo:

welcome to NSSF MOBILE

To register' write the word REGISTER leave space, enter your NSSF ID then send to 15747

>

Karibu NSSF MOBILE,
Kujisajili tuma neno SAJILI acha nafasi, andika namba yako ya NSSF, kisha tuma kwenda 15747

>

Utapata ujembe unaosema:

Welcome NSSF member to NSSF MOBILE!
Send BALANCE to get your balance, STAT. to get STATEMENT. send to 15747

utapatiwa:
your last ten contributions
 
yeah...hata mimi nataka kujua mkuu

KUJUA KIASI ULICHO CHANGIA KWA WANACHA WA NSSF:
Fuata maelezo yafuatayo;

tuma blank text kwenda 15747

Ans.

welcome to NSSF MOBILE

To register' write the word REGISTER leave space, enter your NSSF ID then send to 15747

>

Karibu NSSF MOBILE,
Kujisajili tuma neno SAJILI acha nafasi, andika namba yako ya NSSF, kisha tuma kwenda 15747

>

Utapata ujembe unaosema:

Welcome NSSF member to NSSF MOBILE!
Send BALANCE to get your balance, STAT. to get STATEMENT. send to 15747

utapatiwa:
your last ten contributions
 
Mi nimejaribu lakini sms ya Kujiunga inakataaa kwenda...nimepata sms ya kwanza kuniambia nijiunge...ila majbu yanakataa kwenda....na simu ina credit...sijui tatizo ni nn
 
Back
Top Bottom