Msaada kuhusu mafao ya NSSF..

Msaada kuhusu mafao ya NSSF..

Habari zenu wana jamii?
Naombeni mnisaidie mawazo, nina jamaa yangu mmoja alikuwa akifanya kazi katika kampuni flani hapa mjini (DSM) zaidi ya miaka 10. Ila ameacha kazi na hakuwa kwenye good terms na mwajiri wake wakati anaacha kazi hakupewa barua ya kuachishwa kazi. Anahitaji kufatilia mafao yake ya nssf. Je ni taratibu (procedures) gani anatakiwa azifuate ili alipwe mafao yake? na afanye nini endapo aliyekuwa mwajiri wake atagoma kumsainia papers zinazomthibitisha kuwa alikuwa mwajiriwa katika hiyo kampuni.? Mawazo yenu ni muhimu hapa.

Binafsi kuna mtu namfahamu yalimkuta kama hayo!!
Ukweli jamaa walimwekea ngumu ile mbaya, yaani mwajiri na nssf pia, pesa zenyewe anazodai ni ndogo za mbuzi tu, lakini zilimtesa sana kwa kipindi kifupi!!

Alifanya hv:
1. alienda pale mediation karibu na akiba, akawaeleza abc
2. wakampa barua ya kumuita pale ofcn, akakataa kuja kama mara mbili hv
3. wakamwandikia barua ya kumwita tena, akaja
4. wakaongea weeeeee lakn mwisho wa siku jamaa akatoa barua, tena na vihela kidogo kama compensation. Ila sina uhakika kama case yako imefanana sana na hii

5. baada ya hapo akapeleka barua ya kuacha kazi pale nssf temeke
6. akapewa form ya kwenda kujaza, nadhani zipo tatu hv, kuna sehemu ya kusaini mwajiri, mbunge,serikali za mitaa, nk yeye alisainishwa na serikali za mitaa
7. within three weeks za kupigwa tarehe kachukua mzigo wake kam 2.9m hv, ni nov mwaka jana
8. sijui alihonga baada ya kupewa mzigo wake, ama chuma ulete ama lah, but sasa hv najua zimeisha, zimefanya kazi ya kujenga taifa, mfumuko wa bei balaa mbaya!!
7. sasa hv maisha yake yanaendelea kama kawaida, ameshakula jasho lake!!

Mpe pole sana, but atashinda asiwe na hofu!!
 
Sawa zimefika mkuu! Yah! Naona kama story zinaufanano flani hivi, ila tofauti ni kuwa, huyu jamaa yangu to be honest kuna inshu alifanya then akaamua mwenyewe kutorudi kazini... lakini sasa ameamua kufatilia stahili zake ila alikuwa na uhakika kuwa akipeleka documents kule kazini mwajiri wake atamgomea na hapo ndipo penye utata..Otherwise kwa maelezo ya wadau NSSF hawana shida.
 
na je kuna,njia yeyote ya kujua jumla ya nafao yako bila kwenda ofsin kwao yaani nssf?

Kwa wenye uzoefu huwa wanafanya tracking na payslips zao, lakini sasa hivi ukijiregister kupitia simu, unapata Balance au statement yako ya NSSF. Sasa hivi wako advanced. Lakini kumbuka cm ambayo utaregister ndo utakuwa unatumia wkt wote na wamefanya hivyo ili mtu aciweze kupata data ya mtu mwingine.
 
Hapana kuhusu mafao yoyote Yale (Nssf, Ppf GEPF, pspf, etc) haijalishi uliacha kazi kwa kufuata utaratibu AMA la, lazima ulipwe haki zako na mwajiri hana mamlaka juu ya hilo

Niliuliza maana inaonekana ni dhahiri barua ya kuacha kz hakupewa, kuna watu wanaweza kutuma resignation kwenye email na hawarudi tena kwa mwajiri. Hapo huwezi kumlaumu mwajiri kama wewe mwenyewe hujafika kudai unachostahili. Kingine ni kwamba tukumbuke employee na employer wana rights na obligations.

Advise yangu...Never burn bridges...

Labda barua hajapewa maana kuna vitu vya kampuni hajakabidhi rasmi...
 
mmh basi huku kwetu hatujahamia dijitali!, me nilifatilia last week nikapewa fomu na lazima muajiri wako asaini na barua ya kuacha kazi lazima uwe nayo.

Bado huo ndiyo utaratibu. Na lazima uwe na smartcard kuharakisha mafao yako. Maana kitaratibu inapaswa itoke ndani ya siku 14.
 
KUJUA KIASI ULICHO CHANGIA KWA WANACHA WA NSSF:
Fuata maelezo yafuatayo;

KWENYE SIMU YAKO TUMA UJUMBE MTUPU KWENDA 15747

utapata majibu yasemayo:

welcome to NSSF MOBILE

To register' write the word REGISTER leave space, enter your NSSF ID then send to 15747

>

Karibu NSSF MOBILE,
Kujisajili tuma neno SAJILI acha nafasi, andika namba yako ya NSSF, kisha tuma kwenda 15747

>

Utapata ujembe unaosema:

Welcome NSSF member to NSSF MOBILE!
Send BALANCE to get your balance, STAT. to get STATEMENT. send to 15747

utapatiwa:
your last ten contributions

Umefafanua vizuri saaaaaaaaaaana.
 
... Poa ndugu'
kazi njema.
 
Pole kwa usumbufu!
jaribu tena, kwa kufuata utaratibu na mtiririko mzima. Natumaini utafanikiwa.
Wengi na wote waliokuwa wameniPM, wamerudisha majibu yakufanikiwa. Tafadhari jaribu tena.
Ciao.
 
Pole kwa usumbufu!
jaribu tena, kwa kufuata utaratibu na mtiririko mzima. Natumaini utafanikiwa.
Wengi na wote waliokuwa wameniPM, wamerudisha majibu yakufanikiwa. Tafadhari jaribu tena.
Ciao.

mkuu wanatoa jumla ya nchango yote au inakuwaje? nataka kujua jumla ya michangu yangu yote...
 
Habarini za mchana ndugu, nimefuatilia kwa makini sana maelezo yenu kuhusu NSSF, na nimekuwa na Interest nayo kwani na Mimi nataka kuchukua mapato yangu, ila tatizo langu ni kwamba muda huo wa miezi sita ni Mingi sana kwangu, kwani nataka kwenda shule nje ya nchi. nataka nichukue mafao yangu hayo yaisaide family yangu kabla sijaondoka, ila tatizo ni kwamba niko kwenye mkataba na kampuni moja ya wazungu na mkataba huo unaisha tar 15 april 2013. nami nataka ndani ya mwezi huo niwe nimepata hizo pesa sijui ndugu mtanisaidiaje kwa hilo. Na pia siwezi kupata form ya shule kwa sasa, kwani imeshukia kwa sponsor wangu. naye ameniambia habari za familia yangu nishughulikie mwenyewe na amenipa miezi 2. hebu niambieni kwa undani kuwa nifanye nini ili nipate msaada na kupata fedha zangu kabla ya mwezi aprili kuisha. nitashukuru kama nitapata ushirikiano
 
Suala lako lina utata kidogo, kwanza kabisa suala la miaza sita linaweza kuepukika kwa sababu mbili nnazozifaham mimi:-
1. Kupata shule

Ukiwapelekea admission letter NSSF wanakupa hela yako, kwa kesi yako mesema hauwezi kupata iko kwa mwajiri wako itakuwa ngumu kidogo. Hapo inabidi utafute barua ya admission ya chuo hata kama sio hicho utakachoenda ili ikusaidie kupata hela yako NSSF.

2. Kusafiri kwenda nje ya nchi.

Ukiweza kuwapatia document za kusafiri Visa napo watakupa hela yako with immediate effect.
 
Back
Top Bottom