Msaada kuhusu M-Pesa

Msaada kuhusu M-Pesa

pamoja sana wakuu...bado nasubiri miracles to happen...ntaweka update hapa ili kila mtu ajifunze kitu kuhusu hizi huduma na si kuwalaumu Voda...nasubiri 24 hrs walizonipa ziishe hapo saa saba mchana wasipokuwa wameingiza ntawapigia tena....
 
tatizo ni pesa mingi mkuu....na je account za nmb na crdb zinafanana!? me nilitegemea itaniambia hiyo account haipo!?
Akaunt zinaweza zikawa hazifanani ila unapotuma ela kinachofanyika kwanza ni ile ela inatoka kwenye system ya VODA (MPESA) na kuingia kwenye system ya CRDB then from there ndio inaanza ku-identify akaunti husika. Ni sawa na unavyomtumia mtu Mpesa kutoka akaunti ya bank, kwanza itakuja sms kutoka bank itakwambia tunashughulikia au hamisho la fedha kutoka bank kwenda Mpesa limefanikiwa (lakini haina maana kwamba salio limefika kwa uliyomtumia ikiwa na maana salio limeingia kwenye system ya Mpesa) alafu baada ya dakika 2 tena itakuja sasa sms kutoka Mpesa kudhibitisha yule uliomtumia amepata hiyo ela.

Hapo wakati unasubiri hizo siku saba unaweza ukapiga na CRDB pia zile namba za receipt zinazokuja na sms ni muhimu kuzi note kwani ni sehemu ya kielelezo. (ni rahisi kushughulikiwa kwa simu kuliko kwenda physically kwani itategemea utakutana na nani hapo)
 
pamoja sana wakuu...bado nasubiri miracles to happen...ntaweka update hapa ili kila mtu ajifunze kitu kuhusu hizi huduma na si kuwalaumu Voda...nasubiri 24 hrs walizonipa ziishe hapo saa saba mchana wasipokuwa wameingiza ntawapigia tena....
Subiri mkuu hiyo hela itakuwa inaelea hewani yaani imehamia kwenye system ya CRDB alafu baadae inashindwa ku-identify akaunti, transaction yoyote ukituma kama ukiwahi kupiga simu inazuiwa japokuwa inategemea customer care aliokupoea anaijuaje kazi yake vinginevyo utaipata hata kama itachukua muda
 
sasa mkuu...swali ni kwamba kama account za crdb na nmb hazifanani c ingekuwa hiyo account haipo crdb c ingerudi kama wrong number mkuu...
Account za benki haziwezi kufanana, hujaambiwa kwamba ni wrong number kwa sababu process uliyokuwa unafanya sio real time, kuna delay na kwa sababu ulikuwa umehusisha system tofauti kwa maana system ya Mpesa pamoja na system ya NMB, unapotuma hela haiendi moja kwa moja na kunakuwa na kama fuko la jumla ambalo hela zinakaa hapo na baadaye ndo huenda kwa destination husika, zinazokosa sehemu ya kwenda zinabaki kwenye fuko hilo na ndo maana baadaye kwa wanaozidai zinarudishwa.

Nitoe mfano ambao unahusisha system zote za mobile money, Mpesa na Tigo pesa, nilimtumia mtu wa Tigo kwa Mpesa lakini sikumwambia kama nilimtumia kwa sababu niliamini atapata sms lakini baada ya wiki hela ilirudi kwangu bila hata kuidai.

Kuhusu benki na simu nadhani inabidi uidai kwa sababu mpesa wao watakuwa waliituma kwenda benki ila ingekuwa haijatumwa kwenda benki isingezidi masaa 24. Lakini kukuhakikishia tu ni kwamba hela iliyoko kwenye system haiwezi kupotea na lazima watakurudishia tu, tatizo ni kwamba watachelewesha.
 
Update-Maombi yangu yamejibu wakuu...vodacom wamerudisha muhamala niliokosea juzi baada ya siku moja na nusu...nawapa heko but waboreshe zaidi customer care yao ili ikidhi matakwa ya wateja...nadhubutu kusema bila juhudi zà kuwasumbua kila mahali ingechukua siku saba kama walivyokuwa wanasema but niliwaandikia popote pale walipo kwenye mitandao...heko kwa CRDB bank customer care yao ipo vizuri sana...
 
Wakuu heshima kwenu,

Nilikuwa natuma pesa kwenda bank ya NMB kwa kutumia M-Pesa, bahati mbaya nikachagua CRDB badala ya NMB. Account ni sawa but imeenda bank ya CRDB badala ya NMB. Nimewapigia Mpesa huduma kwa wateja wamesema pesa itaridishwa baada ya siku saba za kazi, na bahati mbaya nipo mbali na ofisi za Voda au bank kwa sasa.

Je, ni kweli itarudishwa au mpaka niende Phsicaly Office za Voda!? Je, inawezekana account ya bank moja ikafanana na ya bank nyingine!?

Naombeni msaada wa mawazo!

Wameshaipiga hiyo, utafuatilia hadi ukome!!!! Pole sana mkuu!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom