Msaada kuhusu kurudia mtihani wa kidato cha nne

Hamna Mkuu ,
Vyeti vyote vinatambulika ndo hasa lengo la kurudia mtihani. Ili kutafta kilicho Bora hila ukikosa unakausha tu
Thanks! Kwenye matokeo yangu kuna F 2 ya MATH na GEO huwa zinanipa kinyaa sana.
Huwa nafikiria kuziondoa ila mwakani nina mpango wa kuacha kazi nifanye mambo mengine, sasa nafikiria nirisiti ili iweje?
Ila kuishi na hili zigo naonaga linanichosha ingawa hajui mtu.
 
Hakuna grades za private candidates pekee, grades zote zipo sawa kama wanafunzi wa shule. Naongea kama mwalimu/mkuu wa shule wa zamani mzoefu na nimehudhuria marking za mitihani mingi ya kitaifa.

Tofauti yao ni kutokuwa na alama endelevu tu ambao wanafunzi wa shule hupelekewa na kuhusika katika uchakataji wa matokeo yao ya mwisho..

Hizo ni nadharia za mtaani tu kwamba alama za wanafunzi binafsi zinakua tofauti na wanafunzi wa shule mkuu. Utofauti upo kwenye CA tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini wengi wanaorudia mitihani wana feli sana?

Yaani kuona one ya PC ni mbinde sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini wengi wanaorudia mitihani wana feli sana?

Yaani kuona one ya PC ni mbinde sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Anayerudia mtihani hawezi akarudia masomo yote saba au nane ili kuweza kupangiwa division! mara nyingi unakuta anarudia masomo matano kushuka chini

sasa ktk mazingira hayo, huwezi kupewa division
 
Simpo tu mkuu, kurudia mtihani maana yake ulishafanya na unataka kujaribu bahati yako kwa mara ya pili.

Unachotakiwa kufanya ni kwenda kwenye shule/kituo chochote kinachoandikisha wanafunzi wa kujitegemea/pc ili upewe namba rejea ambazo kila kituo hupewa na baraza la mitihani.

Kwa kawaida namba hizi huwa bure kwa mujibu wa baraza , lakini andaa elfu 30 mpaka 50 kwa ajili ya kuilipia kwa jina ya gharama ya kituo husika, lazima utatakiwa kulipia gharama hizi katika shule/kituo husika.

Ukipata ref namba unakwenda nayo mara nyingi posta ya karibu wana dirisha linalohusika na ulipiaji wa mitihani kwa wanaorudia.

Gharama za hapo huwa 65 kwa maana ya mtihani elfu 50 na gharama za posta wao huchukua 15.

Posta watakachohitaji; namba yako ya mtihani uliyofanyia awali mfano s4554/6766/2017, kituo unachofanyia, sanduku lao la barua, email kama unayo na masomo unayorudia.

Ukiwapa ndani ya dakika 5 wanaingiza taarifa hizo na kukupatia karatasi yako ya usijali. Unaweza kuitoa kopi ukapeleka kwenye shule/kituo husika kwa rejea ya baadae.

Hapo unakua umemaliza jukumu lako na namba yako ya mtihani husika itatumwa kwenye kituo chako mwezi mmoja kabla ya siku ya mtihani. Utaenda kuichukua kwa mkuu wa shule/kituo katika muda huo tayari kwa kuanza mapambano mapya.

NB: wanaorudia mitihani hawana continuous assessment mana wao sio wanafunzi endelevu wa shule. Unajisomea binafsi au baadhi ya shule/vituo hufundisha kwa mfumo wa tuition. Lakini hata kama utakua darasani na kufundishwa hutakua na alama endelevu, wewe unapambana na paper ya necta tu.

Faida yake, huvai uniform siku ya kwenda kwenye mtihani wa necta. Unatupia chchote kwa mujibu wa tamaduni za Mtanzania unazama mahakamani.

ANGALIZO: Katika kila mtihani kumbuka kubeba ile karatasi yako yenye namba ya mtihani utakayoipata toka kwa mkuu wa shule/kituo mana ndio kitambulisho chako.

Ingawa wasimamizi wanakua na sheet
nyininge toka necta yenye majina na picha zote za watahiniwa, ila nawe ni lazima kuwa na barua yako. Usijaribu kudanganya wana data zote za watahiniwa wa kituo husika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Shukran mzee maelekezo yako yanafaida nyingi Sana mola akubarik sana
 
Anayerudia mtihani hawezi akarudia masomo yote saba au nane ili kuweza kupangiwa division! mara nyingi unakuta anarudia masomo matano kushuka chini

sasa ktk mazingira hayo, huwezi kupewa division
Kwahiyo mkuu yale matokeo tunayoonaga pc wamefeli sana, kiukweli kabisa baadhi yao wanakua hawajafeli masomo wanayorudia!?
 
pia kama wahitaji msaada zaidi, nicheki 0679 168 264
Vipi anaetaka kufuta D yake moja ana uhakika atapata hata C au B anaruhusiwa kufanya mtihani mmoja? Vipi division ile ya zamani inabaki ile ile au inapanda?
 
Thanks! Kwenye matokeo yangu kuna F 2 ya MATH na GEO huwa zinanipa kinyaa sana.
Huwa nafikiria kuziondoa ila mwakani nina mpango wa kuacha kazi nifanye mambo mengine, sasa nafikiria nirisiti ili iweje?
Ila kuishi na hili zigo naonaga linanichosha ingawa hajui mtu.
Ukifanya ukafaulu, vipi ile division ya kwanza inabadilka au inabak ileile? Mfano mtu alkua na II ya 18 then afanye mtihani mmoja apata mfano A au B, division ile ya mwanzo inabak au anakua kapata division I kwa sababu ya somo alilorudia na akafaulu??
 
Back
Top Bottom