Msaada kuhusu kiagiza gari nje na ulipaji gharama

Nyamboboy

JF-Expert Member
Jun 22, 2017
361
451
Ndugu zangu

Kama kichwa cha habari kinavyoeleza hapo juu,Naomba kufahamishwa kuhusu gharama za ziada kwa mtu aliyeagiza gari lake nje hasa kwa Japani.Kuna ndugu yangu ameona gari zuri kalipenda. nimeona kununua na usafiri mpaka Dar es salaam port ni Tsh 5,500,000/= Nimejaribu kuingia TRA kwenye used car valuation susytem nikaona ni Tsh 5,000,000/= Naomba kusaidiwa gharama za ziada niweze kumwambia huyu ndugu yangu mwenye kiu ya gari.

NB:Mimi namiliki gari ila nilinunua show room,kwa hyo sijui utaratibu wa kuagiza nje na ulipaji wa gharama za ziada.
 
Taja aina ya gari kwanza ndo uambiwe kuna gharama za TPA zinategemea ukubwa wa gari, grace period yake ni siku 7, kuna Shippers fees $70, kuna agency fee 250,000 kuna Bima etc kuna service ya gari engine oil, oil filter, air cleaner, matairi etc
 
Asante mkuu,Anataka kuagiza corona premio ya mwaka 2000 ina cc 1760
 
Asante mkuu,Anataka kuagiza corona premio ya mwaka 2000 ina cc 1760
Hio sijui ina CBM( Cubic Metres) ngapi yaweza kua 15 au 16 ila kuna hela fixed ya kulipa ni kati ya 230,000 - 270,000 (hii ni fixed) utalipa hio kama utalitoa gari ndani ya siku saba zikizidi hizo siku ssba utalipa hio fixed amount + storage ambayo inategemea na CBM na wanachaji kwa $ kutegemea na siku za ziada zilizokaa kwa kurahisisha tafuta clearing agent akufanyie hizo shughuli
 
Back
Top Bottom