Msaada kuhusu chuo cha Archbishop James University (AJUCO)-Songea

Msaada kuhusu chuo cha Archbishop James University (AJUCO)-Songea

AJUCO ni college ya St. Augustine University of Tanzania. Ni kweli wanatoa MD. Mwaka wa jana baraza la elimu ya udakitari Africa Mashariki na TCU walifungia vyuo kama vinne ambavyo havikukidhi vigezo wa kutoa elimu hiyo. Vyuo vya private na serikali vilikumbwa na kadhia hiyo lakini AJUCO HAIKUKUMBWA NA KADHIA HIYO. Kwangu mimi naisoma hiyo kama chuo kilichokubalika na serikali. CUHAS Bugando ndio college ya kwanza SAUT kutoa medicine na sasa ni chuo kamili. Kutokana na ushindani uliopo ni vizuri kijana awe na option za kutosha pamoja na hii. Mimi naamini wakati wa kufikiria vyuo ndo huu kwa kuangalia scenario zote za matokeo na kujua vyuo kama mnavyofanya sasa majibu yakitoka ni rahisi kujipanga. All the best.
Shukrani sana mkuu. Umenitoa sehemu moja na kunipeleka sehemu nyingine kwa huu ushauri wako.
 
Nashukuru kwa michango yenu na ushauri mnaonipa. Mumenifanya nirudi katika hali yangu ya utulivu wa akili. Maana alinichanganya kiasi kwamba nilikosa raha.
 
Mzee,

Nikupongeze.

Maana sio kazi rahisi, changamoto ni nyingi mno ambazo naamini umekumbana nazo hadi kijana kumaliza shule.

Pia nimpongeze na kijana pia kwa kuhitimu!

Kuhusu kichapo,

Basi usimtandike tena, ataathirika kisaikolojia, na pia ataweka chuki na wewe.

Naomba ujaribu kukaa nae, uongee nae kama rafiki sasa

Umuulize kwanini anahitaji kwenda hicho chuo.?!

Akikupa sababu zake, nawe umueleweshe kwanini unakipinga na umwambie chuo ambacho unahitaji aende, umpe na sababu zako!

Naamini atakuelewa na atakwenda kwa moyo mmoja.

Ninaongea haya nikiwa kama kijana chini ya miaka 25
Ni kweli kumpiga ni kosa, lakini alileta tabia ambayo hata kuvumilia nilishindwa. Alikuwa anataka nimsikilize yeye tu hataki ushauri. Nikitoka huku nyuma wadogo zake moto unawaka, hasira zinaishia kwao. Hapa ndani ni fujo tu, wakiwasha TV anazima, wakigeukia kucheza games nako tatizo kisa tu apewe uhuru afanye atakavyo.
 
Kweli mkuu kuna kipindi inabidi tujue kwamba mtoto atabaki kuwa mtoto na mzazi atabaki kuwa mzazi haijalishi kiwango cha elimu kilipofikia....kuna wakati huwa tunajisahau sana na kuona kama tumeshafika level ambayo mzazi inabidi akusikilize wewe tuu kitu ambacho sio kweli
 
Ana bahati mbaya amezaliwa na mimi, maana moto wake anajua vema. Nami sipendi hata kidogo kupiga watoto. Huyu nafikiri huko boarding alikokuwa ndio kumempa ujeuri. Nami nimeona nimpashe mara ya mwisho ajue bado sijazeeka akasimulie huko chuoni anakotaka kwenda mkuu. Asijifanye baba kwenye nyumba yangu.
Kuna mzee na mwanae wakianza kuchapana utafikiri ni waume wenza waliofumaniana.ila muamini.maana yeye ndie atakayesoma,mwache akasome anapopenda.kuepusha lawama.
 
Kuna mzee na mwanae wakianza kuchapana utafikiri ni waume wenza waliofumaniana.ila muamini.maana yeye ndie atakayesoma,mwache akasome anapopenda.kuepusha lawama.
Sawa mkuu! Ila nijuavyo hawa vijana wanakuwa bado hawana uelewa mpana sana juu ya mambo wayatakayo. Kumbuka mwaka jana kama sikosei kuna vyuo vingi viliingia kwenye orodha ya vyuo visivyo na sifa. Na wakati huo vilikuwa tayari na wanafunzi, sasa lengo langu nataka tukae tuangalie ni vyuo vipi ambavyo hata tukituma maombi na akachaguliwa kusiwe na wasiwasi tena.
 
Mzee kumbe ndio umekuja kunitangaza huku ulivyonichapa jana

Ha ha ha natania tu mzee wangu

Vijana wengi wenye ndoto za udaktari wameshindwa kwa sababu ya makosa kwenye uchaguzi wa vyuo...Vyuo vizuri vya serikali (MUHAS na UDSM) vinahitaji ufaulu mkubwa

Hivyo basi huenda dogo kaishatabiri matokeo yake so anaandaa mazingira ya kwenda AJUCO ambapo huwa hapana ushindani sana lakini pia ada yake ni nafuu sana ukilinganisha na vyuo vingine vya private
 
Kama angetoa wazo kama hilo wala kulikuwa hakuna shida mkuu.
Angesema hebu tuangalie hata upande wa pili tujue mapema kabla matokeo hayajatoka isingekuwa tabu.
 
Mkuu hicho chuo ni kimojawapo kati ya vilivyopigwa stop kudahili kwa mwaka huu, mwambie dogo afikirie kwingine....
Vyuo vya medicine vilivyobaki ni vichache sana mwaka huu, hivyo inatakiwa kuwa makini wakati unafikiria application.......
 
Back
Top Bottom