CYBERTEQ
JF-Expert Member
- Feb 11, 2012
- 7,341
- 4,074
Mkuu anafungua 100% hata wewe mwenyewe nenda pale kama unashida
wewe utakuwa unazungumzia carrier lock, simu iliyofungwa kwa ajili ya kutumika kwenye mtandao mwingine, icloud lock ni simu iliyopigwa marufuku na server za apple mpaka hapo mmiliki halali atakapothibitika kwa kuingiza iCloud ID na password sahihi! ukijifunza kidogo tu ufanyaji kazi wa apple accounts ungeshajua kuwa haiwezi kufunguliwa kitoto! unahitaji access ya server za apple kuweza kufungua simu ambayo iko icloud locked! developer nguli wa iOS bado wanatoa macho mpaka sasa hakuna solution ya kuikwepa security ya apple. Sasa hivi mtu akinunua iCloud locked iphone atapigia picha, mtaani iPhone 5s zilizofungwa zinauzwa mpaka laki mbili, 5 mpaka laki na nusu, 4s laki moja...we unafikiri huyo erick angekuwa anaweza kuzifungua watoto wa mjini si wangekuwa wanampelekea, tena angepata wateja mpaka marekani! Mtu atakayeibuka na hiyo soliution kama ataamua kutoigawa basi atatajirika ndani ya mwezi mmoja tu, maana hilo ni janga la dunia nzima! Aman Cosmas hebu tuambie vipi "mtaalam" aliweza kukufungulia hiyo simu?
Last edited by a moderator: