Msaada: Kitengo cha Mazingira Mkoa wa Morogoro

Eng Inc

JF-Expert Member
Feb 3, 2017
627
931
Habari!

Niende kwenye topic moja kwa moja.

Watu wenye dhamana ya mazingira mkoa wa Morogoro (NEMC) tafadhali naomba mtusaidie wakazi wa eneo linaitwa Ipo Ipo (Mazimbu), kuna bar inaitwa Diki Diki ni tatizo kwa tunaoishi maeneo hayo kwani ifikapo usiku hawa watu wanafanya uchafuzi wa mazingira kwa njia ya sauti yaani ''noise pollution''.

Tumeripoti kwa Mwenyekiti wa Mtaa, Mtendaji wa Kata na polisi tulienda kufungua kesi lakini huko kote tuligonga mwamba maana mmiliki wa bar hiyo kwa kutumia wadhifa wake (mfanyakazi wa serikali).

Zaidi ya mara 5 tulipopeleka suala hili kwenye vyombo husika huishia kutukejeli na kutuambia hatuwezi kumfanya chochote na isitoshe wameshajimilikisha kwenye hili suala kwa kuleta live band mara tatu kwa juma, tena wanapiga music huo kwa sauti ya juu sana hadi saa 8 usiku. Jambo ambalo ni kero na usumbufu uliopitiliza kwa wananchi tunaoishi maeneo hayo.

Ni dhahiri kwamba mmiliki wa hii bar yupo juu ya sheria sambamba na kuwa juu serikali (mtaa) maana ni muda sasa wananchi tumeripoti na kulalamika bila kupatiwa ufumbuzi wa tatizo hili.

Ninaposema ni ''noise pollution'' ninamaanisha ni pollution kweli kweli na kero zake ni kubwa mno.

Wahusikia na wadau wa mazingira mkoa wa Morogoro najua kwa namna moja au nyingine mpo humu tunaomba msaada wenu hawa jamaa ni dhahiri wapo juu ya sheria na hakuna wa kuwazuia kilichobaki ni shida tunaipata tuishio maeneo hayo.

Msaada wenu wakuu tafadhali.

Samahani mimi siyo mwandishi mzuri.
 
Back
Top Bottom