KERO Bar ipo Sinza Palestina inapiga muziki makazi ya watu mpaka asubuhi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Sinza palestina mtaa wa mpangala -bar inaitwa mwanzo pub ipo katikati ya makazi ya watu inapiga mziki mpaka asubuhi

Anadai yeye ni kigogo vituo vya polisi vya jirani urafiki na mabatini wanambeba sababu mmiliki ni askari aliyefukuzwa kazi

Ameripotiwa serikali za mtaa husika lakini hakuna matokeo chanya sababu wanasema ni kipindi cha uchaguzi wanaogopa kukosa kura wanasema ndio muongozo waliopewa

Tunaomba mamlaka husika za NEmc ziangalie suala hili

Maana ni noise pollution na inatukosesha amani wananchi wa mtaa huu

Hata leo hii mpaka saa saba za usiku tuma maafisa husika utakuta mziki unarindima mtaa mzima

Raia Mwema
 
Hizi pubs na makelele yao ndo zinafanya wagonjwa wa akili wanakua wengi mjini. Mkuu wa mkoa kashasema asietaka makelele ahame Dar. Na makanisa ya walokole washindane na wenye bar na pubs kupigizana makelele atakae choka amuache mwenzake. Kiufupi hakuna anaejali..kilichobaki ni kufunga kuomba isitokee jirani na kwako mtu akaweka pub,au walokole wasijenge kanisa
 
Back
Top Bottom