Well, ushauri wangu hauwafai...
Watu wanaumwa kwa sababu tatu:
- Mabadiliko ya mwili kikemikali yanayosababishwa na mwili wenyewe, vimelea vya magonjwa au vichoheo vya kawaida vya nje, haya huleta magonjwa ya kawaida kama Maleria n.k ambayo hutibiwa kwa dawa na vifaa tiba vya kikemikali, iwe hospitali za magharibi, za kiafrika au za namna nyingine.
- Mambo ya Kiroho: Kwa kusababishiwa na watu, kukutana na mapepo bahati mbaya na kadhalika na huweza kusababisha madhara ya kikemikali mwilini. Ndio, unaweza kulogwa, kukutana na pepo na ukaumwa ugonjwa wa kawaida kabisa, changamoto yake ni kuwa kupona kwa dawa za kawaida ni changamoto.
- Kusababishwa na nguvu kuu: Miungu na mizimu huleta magonjwa kama njia ya kuonya, kutahadharisha, kulipa kisasi na wakati mwingine kushinikiza mambo fulani miongoni mwa binadamu.
Kila namna ya kuingia kwa ugonjwa una namna yake ya kutoka na isiyofanana wala kufanya kazi kwenye mazingira tofauti: Ukiumwa Homa ya Plasimodiamu kisha ukaenda kanisani au kwa mganga wa kienyeji unakufa huku unaona, na kinyume chake. Ubaya ni kuwa madakitari wa mrengo mkuu hawakubali kuwa namna zao zimefeli katika mazingira fulani, kila siku wana majibu mapya, matumaini mapya na yote yanafeli, kisha mzunguko ukarudi mwanzo.
Nionacho mimi ni kuwa dogo anaangukia katika makundi mawili ya mwisho, aidha wamemtupia madudu, au ni mambo ya miungu na mizimu. Kutibu kwa namna moja kunafungua njia ya kufahamu cha zaidi kinachomsibu - Nashauri mfanye tambiko kwa mizimu yenu, mtoe sadaka ya upatanisho kwanza: kwa mizimu kuokoka ni kuasi!
Baada ya hapo mnaweza kutoa sadaka zingine kadiri yamaelekezo mtakayopewa na kuhani wa kabila lenu. Huo ni mwanzo na utatoa mwanga mzuri wa kinachomsibu mwanenu.
Mizimu yenu iwape kibali!