Msaada kesi ya mirathi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada kesi ya mirathi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Adm, May 8, 2011.

 1. A

  Adm Senior Member

  #1
  May 8, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 150
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mimi nilifiwa na mzazi wangu wa kiume ambaye alikuwa mwajiriwa serikalini. Baada ya mazishi kikao cha wanandugu kilimteua baba mdogo kama mfuatiliaji wa mirathi. Lakini tangu kuteuliwa kwake huyo baba mdogo hafuatilii waa haonyeshi juhudi zozote. Swali kwenu ndugu zangu wana jf,SHERIA INASEMAJE KUHUSU KUMBADILISHA MSIMAMIZI WA MIRATHI ENDAPO ALIYEPO HAONYESHI KUWA ACTIVE? Naombeni msaada kwa hilo kwa mwenye uzoefu wa kesi hiyo ama mwenye ufahamu wa sheria juu ya hilo
   
 2. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2011
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,753
  Likes Received: 555
  Trophy Points: 280
  Pole sana,

  Mtu ateuliwapo kuwa msimamizi wa mirathi anayo majukumu,ya kukusanya mali za marehemu,kulipa madeni anayodaiwa marehemu,pamoja na kugawanya mali kadri wosia wa mareehemu utakavyokuwa unaelekeza.Msimamizi huyu lazima ahakikishe anaendana na matakwa ya wanandugu waliomteua pamoja na amri ya mahakama iliyomdhibitisha.Ikiwa ataenda kinyume na matakwa hayo,basi wewe kama mmoja wa warithi,unayo haki ya kwenda mahakamani na kuweka pingamizi juu ya mwenendo wa msimamizi huyo,kama unazo sababu za msingi basi mahakama itatengua uteuzi wa msimamizi huyo na kumteua mtu mwingine ukiwemo hata wewe mwenyewe kuendelea na majukumu aliyokuwa nayo msimamizi wa awali.

  Utaratibu juu ya kuweka pingamizi umeelezwa vizuri katika sheria ya Mirathi.Tafuta Wakili yeyote akuelekeze.
   
 3. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,521
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Pole ndugu. Lakini kabla ya ku resort matumizi ya mahakama, nijuze juu ya mambo yafuatayo: mzazi wako alikuwa ni mwajiriwa Serikali Kuu au za Mitaa? Je huyo ndugu yako alishajaza fomu za kudai mafao ya pensheni? Je mnaishi wapi hapa bongo?
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Pole mkuu, kwanza utaratibu wa kuteua msimamizi wa mirathi sijui kama ulikuwa sawa. Ninavyojua mimi akifa mmoja wa wazazi basi anayebaki ndo msimamizi wa mirathi. Mama yako bado yupo? Kama yupo basi kihalali ndo msimamizi wa mirathi, kama hayupo basi watoto wenyewe ndo mnateua msimamizi wa mirathi miongoni mwenu, huyo aloteuliwa ni mwangalizi wa familia tu kimila na si msimamizi wa mirathi nadhani terms hapa ndo zilikosewa, kama waliandika hivyo basi mnaweza kwenda mahakamani kufungua jalada la kubadili msimamizi wa mirathi na kumteua mwingine. Kimsingi ndugu wa karibu hawahusiki na mirathi isipokuwa watoto na wazazi.
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  May 13, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Unachokisema sio sahihi kabisa.

  Kwa mujibu wa Sheria za tanzania, msimamizi wa mirathi ambaye anatambulika kisheria ni yule ambaye mara baada ya kifo cha marhum basi ndugu wote waliomuhusu ikiwemo pamoja na warithi wataakaa kikao chenye ajenda ya kuchagua msimamizi wa mirathi.

  Mkutano huo utakuwa na mwenyekiti na katibu wa kuratibu na kuandika muhtsari na muhudhuriaji atatakiwa kutia sahihi muhtasari huo. ndani ya kikao hicho atachaguliwa msimamizi wa mirathi naye atapitishwa na wajumbe wote kisha nakala ya muhtasari huo utapelekwa mahakamani na picha na death certificate na ushahidi mwingine na kuomba mahakama imthibitishe kisheria kama yeye ni msimamizi halali wa mirathi ya marehemu yule.

  Msimamizi anaweza kuwa mama, Mtoto akiwa na zaidi ya umri wa miaka 18 and ndugu yeote atayechaguliwa na kikao hicho.
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  May 13, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0

  Kwa mujibu wa suala lako, Unayo haki kisheria kama mmoja wa warithi kwenda mahakamani pale pale mlipofungulia mirathi yenu na kuweka pingamizi kwa msimamizi w mirathi na kutoa sababu zinazokufanya usiridhike na utendaji wa huyo msimamizi.( kuna fomu maalum utajaza kisha mtapangiwa siku ya kusikilizwa pingamizi lako na kama litakubaliwa basi Mahakama itatengua uteuzi wa huyo msimamizi wa mirathi na hivyo mtatakiwa kuchagua msimamizi mwingine.

  Hivyo hiyo ni haki yako, nenda mahakamani kaweke pingamizi na utoe sababu za pingamizi lako za kutoridhishwa na utendaji wa msimamizi wa mirathi yenu.
   
 7. L

  Loloo JF-Expert Member

  #7
  May 25, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 214
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  sio kuweka pingamizi pingamiza linawekwa wakati kesi inasikilizwa au kabla hajateuliwa unachotakiwa kufanya ni kuandika barua ya kuomba kumuondoa msimazi wa awali na unaelezea sababu za kutaka atolewe.mahakama itapanga siku ya kusikiliza.msimamizi wa mirathi ni mtu yoyote yule kikao cha ukoo kitamwini na kumteua sio lazima ndugu
   
 8. T

  Taso JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 460
  Trophy Points: 180
  Ni kwa sababu yeye hana chake hapo.

  Na ndio maana watunga sheria waliliona hili zamaaaaani, ikaandikwa kwamba kama marehemu hakuacha wosia basi msimamizi wa mirathi ni lazima awe mmoja wa watakaonufaika na urithi huo. (Probate and Administration of Estates Act,
  1963, CAP 352, Sect 33).

  Na kisheria Baba Mdogo hayumo katika warithi iwapo nyinyi watoto mpo na mjane. (
  J.A.L.A. Cap 358 ss. 14-21, The Indian Succession Act, CAP 358, X-1865. Sect 27-30).

  Kwa hiyo kama mkifanikiwa kubadilisha (ambayo inaweza kuwa si rahisi), basi teueni mtu ambae ana maslahi na mirathi hiyo, mmoja wenu watoto na mama. Baba Mdogo wa nini?
   
 9. hakiyako

  hakiyako Senior Member

  #9
  Jan 11, 2015
  Joined: Aug 24, 2014
  Messages: 148
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  umeongea vyema sana. pia waweza kubofya hapa kwa wale wanaohitaji vitabu. SHERIA TANZANIA
   
Loading...