The Finest
JF-Expert Member
- Jul 14, 2010
- 21,605
- 6,097
SAWEBOY I like your ideaMkuu pole kwa hayo yanakukuta. Kwa kuwa anasema kama umemchoka umwambie tu hapo lazima kuna jambo limejificha na wala usidhani masihara, kuna kitu anajivunia tu na wewe anakuona kwa sasa huwezi kumbabaisha especially kama kuna mtu pembeni na hiyo ni ngumu wewe kujua. Kwa kujihami usijue ndio maana anakujia juu coz ameshajua udhaifu wako kuwa akikupnadishia wewe unaua soo kwa kuwa mpole.
USHAURI MZURI
1. Wewe ndiye uliyemfungulia biashara anayofanya na kupata kipato kizuri tu, pia usafiri umempatia (ana bahati sana ya kupendwa ila hapendeki huyu dada) kwa hiyo hakuna tatizo la wewe kumuogopa, hapo unaibiwa mkuu lazima kuna mtu ana-msugua pembeni bila wewe kujua. Chukua hatua haraka mkuu/ tena faster! Hatua gani sasa ya kuchukua?
2. Mtegee ishu kidogo tu, muulize kwa upoleeee kabisa akikujia juu, we ni mwanume na ndio uliyemuoa hivyo mrudishe kwao kwa mapunziko bila kumwambia lini utamfuata au mwambie rudi nyumbani kwenu na utakapoona umebadilika tabia na kutambua mimi ni mume wako hapo ndipo urudi lakini usirudi kabla ya miezi 6 au 3 hata kama akijua kosa lake!
3. Endapo ukiona amefurahia kurudi kwao na huku anakujibu kwa jeuri basi ujue hapo huna ndoa mkuu lazima ujue kuna mtu anachakachua tu hiyo kitu but ukiona anakuwa mpole ghafla usibadili uamuzi muache aende akajifunze na akirudi kuja kutubu hatarudia tena.
NB: akifurahia kurudi kwao basi ndani ya mwezi 1 utajua nani anasugua huyo mashine na hapo ndo utajua jeuri ya mkeo inatoka wapi.
Pili usimruhusu kuondoka na mtoto, mwambie aende na mtoto amwache home lkn akilazimisha basi muachie mtoto aende nae!
CHUKUA HATUA HARAKA SANA MKUU
mtafutie nyumba ndogo....saa nyengine tunakuwaga na kiburi tukiwa hatuna ushindani,:bange::bange::bange:
Wanawake wengine bwana, watu wanatafuta waume wa kuwauliza tu za kazini hakuna, yeye kapata mume ,kafunguliwa biashara, na bado hata hampi feedback mumewe, lol natamani nimjue nimpe darasa namna ya kuishi na mume mwaminifu kama wewe. Kuwa imara wakati unamuuliza mkazie macho ili akuone una maanisha na hakuna mzaha. Eti sio sie tunataka kujua mume anapata sh ngapi , na vitega uchumi vyote? inakuwaje sie hatutaki kuwajulisha vyetu? Mie hata sielewi kabisa
Kuhusu marafiki vumbi kasema yote na kama humuoni na rafiki basi labda hana marafiki
na yeye kifanya revenge utahimili??mtafutie nyumba ndogo....saa nyengine tunakuwaga na kiburi tukiwa hatuna ushindani,:bange::bange::bange:
PENYE MITI KWELI HAPANA WAJENZI,
Swali la Pauline la mnaishije? ni zito sana,kupitia jibu lako unaweza kupata,
kwa nini huyo mkeo anaanza jeuri ktk kipindi kifupi sana cha ndoa yenu,
pia swali la nyumba kubwa, je uelewa wake ukoje?,nalo ni muhimu sana
Isiwe ni aina ya mwanamke anayechukulia kupendwa kama silaha ya kumnyanyasa mwanaume.
Usitafute nyumba ndogo, bali ongea naye pamoja na watu wenu wa karibu mnaowaheshimu, asipokuelewa mpe muda akapumzike kwao kidogo akiwa huko kama hana mpenzi wa pembeni basi atajirekebisha.
KILA jambo likizidi lina ubaya wake Yawezekana upole wako umezidi kipimo, so yeye anauchukulia ndivyo sivyo kabisa.
Natamani kama ungekuwa wangu.....lol
HONGERA SANA UAMINIFU WAKO,NA ENDELEA KUWA MWAMINIFU NA KUIHESHIMU NDOA YENU, NAAMINI HILO NI WIMBI TU LA KUPITA KUWENI MAKINI,
LISIJEZAMISHA NDOA YENU. POLE SANA, USIPATE PRESSURE ILA HAKIKISHA UNALIPATIA UFUMBUZI HARAKA.
waoo,natamani nipate mume kama wewe...inaelekea umstraabu sana,sijui ufanyeje but you can try kuwaita wazee au wamama anaowaheshimu waongee naye na kumuambia hilo jambo hupendezwi nalo.........au tafuta muda abao mko wote happy,mmerelax umwambie kwa upole kuwa hupendi tabia yake ya kujikweza kama anakupenda atakusikiliza,ila huyi bidada inaelekea anasumbuliwa na pepo la ubinafsi na kujikweza,muombee yatoke lol
ndugu yangu kwanza pole.pili hongera kwa ujasiri na busara ktk hiyo issue.kuwa mpole sio ujinga.Biblia inataka wanaume kuishi na wake zao KWA AKILI na ndo ulivyofanya! Ushauri 1.usimrudishe kwao 2.nahic nawe umechangia hali aliyo nayo mkeo maana km had leo hujui aina ya rafiki wa mkeo napata shida kujua mwanzo wa uchumba wenu ulikuwa wa aina gani.3. Tafuta kitabu kiitwacho NDOA YANGU,NINGEJUA kitakusaidia sana kujua wapi umechangia tatizo lako na kwanini ndoa nyingi hazina amani na zinavunjikaWakuu. Mawazo yenu nayathamini mnanipa faraja. I will soon take a hardline decision naona nyumba inataka kuwa ndogo and I am not prepared. Nina value ndoa lakini I don't give damn a shit! Wacha nimweke under probation for a while or else atajikuta kwao. We only live once na tunataka tuishi kwa amani na raha. Naendelea kuwasikiliza idea zenu ni helpful kwa kweli
Nimependa huu ushauri. Chukua nafasi yako kama mwanaume. Usimbembeleze, anaonekana sio mwelewa.Simama kama mwanaume muulize panapotakiwa kuuliza,asipotoa ushirikiano kuwa mkali kama akizidisha ukorofi funga biashara yake,wewe ni mwanaume lazima uwe kiongozi wa familia!
Nimependa huu ushauri. Chukua nafasi yako kama mwanaume. Usimbembeleze, anaonekana sio mwelewa.