Msaada: Kanguru wanafukua mahindi shamba lote

Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
2,065
2,000
Jamani dunia inamajaribu kila ukijaribu kujikwamua kinaibuka kikwazo ufeli, Kunguru wanafukua mahindi yanayoanza kuota, wamekula shamba zima.

Mwaka Jana panya walikagua kula mstari na kula mahindi yote niliopanda.Msaaada wa kuwadhibiti hawa viumbe.

Panya nilijaribu kumwaga mahindi ya sumu hawakula na wakila wanamenya ganda la nje hivyo waliwin battle, this year kunguru doa.

Kuna sehemu ninashamba kubwa ila nashindwa kupanda kuhofua mapanya na kwale kufaidi nguvu zangu, hivyo shamba 20acre virgin land limelala mwaka 2.

Nafikiria nifanyeje bado sijui jinsi ya kudhibiti hawa pests.MSAADA wa kiufundi.

Thanks.
 
barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
29,785
2,000
Dah..
Pole. Hii inaitwa MCHANA NZI USIKU MBU.
Kuna vitu wakula hasa wa mwanzo huwa tukijazwa upepo na motivational speakers tunaingia kichwa kichwa.
Shirikisha wataalam wa kilimo na piq historia ya wenyeji wa eneo hilo huwa wanakabiriana na hii changamoto viti.
Ila pole mkuu, 'wachawi' wengi sana kila unapojaribu kutoboa wao wanaziba..
 
Mwanamena

JF-Expert Member
Feb 4, 2020
575
1,000
Sio mmoja wamealikna ukoo wote.
Ushauri mzuri ni kuwa, ulizia wenyeji, tafuta waelewa, wengine Wana Roho za kwanini, huwa wanashughulika vipi na hao kunguru.

All in all kumbuka shambani kuna michezo michafu pia, sijawahi sikia kunguru kufukua mahindi yaliyoota, Kware sawa. Rafu za kwenye uchaguzi, mpira wa miguu, huko nako ziko Sana. Pambana kiroho na kimwili pia
 
neez

Member
Mar 4, 2018
99
125
Tafuta ile mikanda ya video ya zamani chukua ule uzi wa ndani chomeka miti kuzunguka shamba af ufunge upepo ukivuma unatoa mlio so wataogopa ile saitipia katikati ya shamba simamisha miti kwa umbali af tundika manguo nguo watahisi mtu hawatatua
 
Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
2,065
2,000
Watu wengine mna habari halafu mnazikalia.. ita vyombo vya habari! Kunguru kula mahindi hiyo ni "breaking news"
Kwa hio niite press conference.
Tafuta ile mikanda ya video ya zamani chukua ule uzi wa ndani chomeka miti kuzunguka shamba af ufunge upepo ukivuma unatoa mlio so wataogopa ile saitipia katikati ya shamba simamisha miti kwa umbali af tundika manguo nguo watahisi mtu hawatatua
Saw a nitajaribu japo kupata hizo tape kazi.Bado zipo mafukami kweli?
 
Tangantika

JF-Expert Member
Aug 12, 2018
2,065
2,000
Ushauri mzuri ni kuwa, ulizia wenyeji, tafuta waelewa, wengine Wana Roho za kwanini, huwa wanashughulika vipi na hao kunguru.

All in all kumbuka shambani kuna michezo michafu pia, sijawahi sikia kunguru kufukua mahindi yaliyoota, Kware sawa. Rafu za kwenye uchaguzi, mpira wa miguu, huko nako ziko Sana. Pambana kiroho na kimwili pia
Mkuu ninavitu vizito,siraha za maangamizi nimepewa huko mwishi wa reli, tatizo shamba sio langu na vitu vyenyewe ni vya kudumu, nataka nikasimike shambani kwangu ambapo ni mbali sana na bado sijapaendeleza.
 
Zesh

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
15,027
2,000
Anayejua zinakopatikana mbegu za nyanya kutoka kampuni ya Kibostar au Safa na bei zake tafadhali anijuze
 
Che mittoga

JF-Expert Member
Mar 28, 2017
5,467
2,000
Kabla ya kupanda, chovya baadhi ya Mbegu za mahindi kwenye dawa ya dudu killer, au DDT, au Kimatila alafu zitupe juu ya matuta au popote zinapo onekana ndani ya shamba lako.
Watazila watakufa wote baadae watalikimbia shamba.
Kila ukipanda endelea kutuba baadhi ya hizo mbegu sumu. Hadi waishe wote.
 
Mkuu siwezi fungwa nikiu 100, maana wapo ukoo mzima na koo za majirani.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom